Watuhumiwa wavurugu hizo wakipandishwa kwenye gari la polisi. Picha na Mtaa kwa Mtaa Blog
Baadhi ya vizuizi vilivyowekwa na waislam eneo la Mbagala Kizuiani wakati wa maandamano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo kupinga kitabu kitakatifu cha Koran kufanyiwa dhihaka na mtoto Emmanuel Josephat ambaye aliitemea mate.
Polisi wakiwa katika kuhakikisha hali ya usalama inaimarishwa katika eneo la Mbagala
Mmoja wa waandamanaji akiwa amekamatwana askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU)
Baadhi ya magari yaliyoharibika katika maandamano ya waislam
HAMISI SALUM BABA MZAZI WA KIJANA AMBAYE MSAAFU WAKE ULIFANYIWA DHIHAKA NA EMMANUEL JOSEPHAT NA KUZUA MAANDAMANO MAKUBWA YALIYOFANYWA NA WAAISLAMU JIJINI DAR LEO.Picha na Happy Mnale
DAR ES SALAAM, Tanzania
VURUGU kubwa zimezuka baada ya mtoto Emanuel Josephat(14)’ kukojolea kitabu cha Quraan cha dini ya kiislam limeingia katika hatua nyingine baada ya waamini wa dini ya kiisilam kukusanyika wakishinikiza kuachiwa kwa mtoto huyo ili wamuue.
Waamini hao wanaokadiriwa kufikia idadi ya 3000 baada ya kutawanywa na Polisi waliingia mitaani na kuchoma kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT), Mbagala Zakhem, Kuharibu Kanisa la Anglican,kuvunja vioo katika kanisa la Wasabato, huku kanisa la Tanzania Assembly of God(TAG), Mbagala Kizuiani wakilichoma moto na kuchukua vifaa vya muziki na kuviunguza hadharani.
Vurugu hizo zilizotokea jana jijini Dar es Salaam, majira ya saa 5 asubuhi ambapo waislamu hao walivamia kituo cha polisi Maturubai,Mbagala Kizuiani.
Vurugu hizo ambazo zimesababisha gari za polisi namba T142 AVV,PT 0966 na T 325 BQP,basi la uda na gari la waandishi wa habari kutoka Clouds zikiharibiwa kwa mawe na waandamanaji hao.
Awali waamini hao walikusanyika katika kituo hicho cha polisi wakimtaka mtoto huyo ambaye alikuwa chini ya ulinzi aachiwe na Polisi walipogoma kufanya hivyo ndipo vurugu hizo zilipoanza.
Kikosi cha kutuliza ghasia kilionekana kuzidiwa nguvu na watu hao ambao walikuwa wakiwatawanya kutoka eneo moja wanakimbilia eneo lingine na kuleta madhara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufunga barabara.
Hatahivyo baada ya viongozi wa dini hiyo kufika wakiwa wameambatana na Sheikh wa Wilaya ya Temeke, Sheikh wa Taasisi na Jumuiya za Waislamu kukaa kikao na kamanda wa Polisi Wilaya ya Temeke, David Misime, walifikia muafaka wa kuwaita waislamu hao na kuwatuliza lakini hali iliendelea kuwa si shwari kwani baada ya viongozi hao kuona waandamanaji hao wakikamatwa na kupigwa walikuja juu na kutishia kuondoka.
“Ndio nini sasa sisi tupo hapa kwa kuleta suluhu lakini ili waislamu watulie lakini mnawapiga mbele yetu ndio nini sasa
|
No comments:
Post a Comment