Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limemkatia umeme Afisa Forodha Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Samwel Kihimbi, baada ya kubainika kuliibia nishati shirika hilo zaidi ya mara moja.
Kabla ya afisa huyo kukatiwa umeme, wafanyakazi wa Tanesco pamoja na askari polisi wa kituo cha Kawe walijikuta katika wakati mgumu baada ya wafanyakazi wa kigogo huyo ambaye ni mkazi wa Mbezi Beach kugoma kufungua mlango.
Hali hiyo iliwagharimu kukaa zaidi ya saa moja getini, huku wakisubiri kibali cha kigogo huyo kuwaruhusu kuingia ndani kwa ajili ya ukaguzi wa mita.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakati wakifanya ukaguzi wao wa mita kwa lengo la kubaini wezi wa umeme, Afisa Usalama wa Kanda Kaskazini Wilaya ya Kinondoni, Shami Dunia, alisema wameamua kumkatia umeme kwa kuwa awali alichakachua mita yake na kujirejeshea umeme pasi na kuruhusiwa na Tanesco.
Alisema Julai 23, mwaka huu, walimkatia umeme baada ya kubainika kuliibia shirika hilo na kutozwa Sh. milioni 6.8 ikiwa ni faini pamoja na malimbikizo ya gharama za umeme tangu alipoanza kuchezea mita hiyo ili matumizi yake yaonekane madogo.
Dunia alisema kigogo huyo badala ya kulipa gharama hizo alizotakiwa na Tanesco, alitumia njia zake kinyemela kujiingizia umeme huku akijua ni kinyume cha utaratibu.
“Hakutakiwa kujiingizia umeme baada ya kukatiwa, kwani ni makosa. Alitakiwa kuja kulipa deni lake na sisi tukamrudishie. Yeye ametumia njia zake kujifungia. Sielewi kama alitumia kishoka, kwani hakutumia utaratibu unaotakiwa huku akijua anadaiwa,” alisema Dunia.

CHANZO: NIPASHE
2 comments:
ndo tanzania yetu hii ufisadi kwenda mbele na katu abadan hatukomea hapo huu ufisadi walio matajiri wana zidi kutajirika na mafukara kunyanyasika,kigosi kachukuwe umeme tena bwana nchi yako hii kila mtu anafanya anavyo weza ili maisha yande ya kifisadi
Mh mi napita tu
Post a Comment