ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 12, 2012

MWENDESHA BODABODA AGONGWA MAKUTANO YA BARABARA ZA KILWA NA MANDELA

Wasamaria wema wakimsaidia Mwendesha Bodaboda ambaye ambaye jina lake
halikupatikana mara moja kutokana na kupoteza fahamu mara baada ya kugongwa na Daladala lenye namba za usajili T 681 ATX linalofanya safari zake kati ya Mbagala na Kariako katika makutano ya barabara za Kilwa na Mandela asubuhi hii jijini Dar es salaam.
Hapa akiwa amelala huku akiwa amepoteza fahamu.

Askari wa kikosi cha usalama barabarani akiamuamuru dereva wa Daladala hilo 
kulipeleka kituoni kwa ajili ya hatua mbalimbali za kisheria kutokana na kutokea kwa ajali hiyo.

Picha kwa hisani ya Dar Es Salaam Leo

No comments: