Mwalimu Mwakasege amingia jana Washington, DC na leo Ijumaa November 23, 2012 kuanzia saa 4 asubuhi ET ameongea na viongozi mbalimbali wa dini kutoka majimbo mbalimbali waliofika Washington, DC tayari kuanza semina itayoaanza leo jioni kuanzaia saa 10 jioni (4pm ET) kwenye hoteli ya Hiilton iliyopoa Greenbelt, Maryland 7810 Waker DR, Greenbelt, MD na Jumamosi itaanza kuanzia saa 2 asubuhi (8am ET) mpaka saa 4 usiku (10pm ET) na Vijimambo itawarushia LIVE hiyo Jumamosi November 24, 2012.
Jackson Mollel kiongozi kutoka Minnesota akiongea machache na kutoa utambulisho kwa viongozi wengine walifika Washington, DC kutoka kila kona ya Amerika.
Mchungaji Malekela akifungua mkutano kwa maombi.
Mchungaji Mngodo kutoka Minnesota ambae ndie aliyekua mshereheshaji kwenye mkutano huo nae akiomba kabla ya mkutano kuanza.
Ps. Samson Ananiah kutoka Minnesota akiimba wimbo akishirikiana namchungaji Malekela kutoka Washington, DC kabla ya mkutano kuanza.
Juu na chini ni Viongozi mbalimbali wa dini kutoka majimbo mbalimbali yaliyopo hapa Marekani wakiwa kwenye mkutano na Mwalimu Mwakasege uliofanyika leo Hilton Hotel Greenbelt, Maryland.
No comments:
Post a Comment