Pati kama hii zilishawahi kufanyika zamani na ziliweza kuwajumuisha Watanzania kutoka sehemu mbalimbali hapa Marekani na wengine wakitokea Canada kwa lengo la Watanzania tuliopo nje kusherehekea kuaga mwaka na kukaribisha mwaka mpya tukiwa pamoja kama Watanzania tulioshikamana wa mzazi mmoja aitwae ughaibuni.
Hili ni jambo jema na linalostahili kuungwa mkono na kila Mtanzania aliopo Marekani na kitu kingine ambacho ningependa kuukumbusha Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV na Ubalozi wetu Washington, DC wasisahau Kualika viongozi wa Jumuiya zote pamoja na Watanzania waishio kwenye Jumuiya hizo kwa lengo la kukutanisha Watanzania waliopo Marekani na kuonyesha umoja na mshikamano wetu.
Jambo lingine ambalo kama inawezekana kuwapunguzia kiingilio Watanzania watakaokuja kutoka nje ya DC kwa lengo la kuwapunguzia gharama kwa mfano nimeona kwenye Flyer inasema $10 Before 11:30 pm na $20 after 11:30 pm. Kwa kuwapatia nafuu Watanzania wenzetu watakaosafiri toka mbali wao wangelipa $10 all night na Watanzania wa DMV wao ndio wangelipa hiyo tofauti ya bei na utawatofautisha kwa vitambulisho vyao.
Hayo ndio maoni yangu na nimatumaini yangu Watanzania wenzangu watalichukulia swala hili kwa uzito unaostahili na hatimaye kufanikisha shughuli hii.
Asante
Mdau DMV
No comments:
Post a Comment