ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 23, 2012

Mwanamke anayetuhumiwa kumtesa kumlisha kinyesi na kumchoma moto mtoto wa kaka yake kumfungia ndani, amepandishwa kizimbani kwa mara ya pili

Mtuhumiwa Wilvina Mkandala (24)
Hataki kabisa kuonyesha sura yake
Aneth akiwa na wazazi wake mahakamani jana
Akirudishwa tena rumande mpaka tena tarehe 27/11
Baadhi ya akina mama wakiwa nje ya mahamaka wakisubiria kumwona mama huyo mwenye roho mbaya
Akina mama hao wakiwa na hasira kali walisikika wakisema tuachieni kidogo tumfunze adabu

MWANAMKE anayetuhumiwa kumtesa kumlisha kinyesi na kumchoma moto mtoto wa kaka yake kumfungia ndani, amepandishwa kizimbani kwa mara ya pili katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya kujibu
shtaka linalomkabili.
Mwendesha mashtaka wa Serikali, Achiles Mulisa ameileza Mahakama kuwa Mtuhumiwa Wilvina Mkandala (24) Mkazi wa Majengo jijini humo alitenda kosa la kusababisha majeraha akiwa
na nia ovu ambayo imemsababishia ulemavu mtoto Aneth Gasto (4).

Mulisa akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo Gilbert
Ndeuruo amesema kosa hilo ni kinyume cha kanuni ya adhabu kifungu cha
222(a) sura ya 16 kama ilivyorejewa mwaka 2002.

Kutokana na hali hiyo mwendasha mashitaka huyo ameileza mahakama kuwa kesi inayo mkabili mwanamke
huyo ilihitaji mashahidi sita ambao ni Dactari aliye mfanyia upasuaji mtoto
huyo mwenyekiti wa Mtaa na barozi wake pamoja na Askari
mpelelezi wa kesi hiyo na mtoto mwenye .

Amesema tayari mashahidi wanne kati ya sita wamekwisha toa ushahidi wao mahakani hapo .

Kutokana na kosa hilo mshtakiwa amekana shitaka hilo ambapo alirudishwa mahabusu hadi
Novemba 27 Mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Amesema upande wa Jamhuri unamashahidi wanne ambao watatu kati yao teyari wamekwsha toa
ushahidi wao katika mahakama hiyo .

Amewataja mashahidi hao kuwa ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Shuku Mwakanyamale, Daktari
anayemtibu mhanga katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya Dr. Paul Kasubi na Habiba Mwakanyamale .

Wengine ni Askari Polisi aliyepeleza kesi hiyo WP Pudensia na Mtoto mwenyewe ambao wako tayari kufika mahakamani na kutoa
ushahidi wao mbele ya mahakama.

Awali mshatakiwqa huyo aliieleza mahakama kuwa na uhusiano na mtoto huyo ambapo
pia alikiri kuwa na taarifa za kile kinachoendelea juu ya matibabu ya mtoto huyo
na kuhusu kukatwa kwa mkono wake wa kushoto na kufungwa bandeji ngumu(POP)
kwenye mkono uliobaki.

Mbeya Yetu

No comments: