Thursday, December 6, 2012

MWANDISHI KUPIGWA RISASI


Ndugu wapendwa,
DSM City Press Club imepata taarifa  za kushtusha kufuatia ya kupigwa
risasi  na kujeruhiwa begani kwa mwandishi wa Tanzania Daima Bwana
Shabani Matutu (30) ambaye pia ni mwanachama wa Dar City Press Club
(DCPC). Sambamba na taarifa hizo imeelezwa kuwa mwandishi huyo
amelazwa katika Taasisi ya mifupa katika hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MOI). Chanzo hasa cha kupigwa risasi kwa mwandishi huyo
bado hakijaeleweka kwa DCPC, uongozi wa DCPC unafuatilia.

Tutakapojiridhisha na taarifa zilizotolewa pamoja na zile
tutakazozipata tutawataarifu rasmi. Kwa sababu hizo tunaomba waandishi
wote, ndugu, jamaa, marafiki, wapenda haki na amani , wanaharakati
washirika na wadau wote wa vyombo vya habari kuwa watulivu tukimjulia
hali kwa misaada ya hali na mali mwandishi mwenzetu Shabban Matutu ili
apone majeraha.
Wenu katika ujenzi wa Taifa,
Joseph Kayinga
Katibu Mkuu

No comments: