ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 17, 2013

MZEE MKAPA NA MZEE MSUYA WATOA MAONI YA KATIBA

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akibadilishana mawazo na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Jan 16, 2013). Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu leo jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa (kulia) akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani (katikati) na Dkt. Salim Ahmed Salim. Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu leo (Jumatano, Jan 16, 2013) jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Cleopa Msuya akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu mchakato wa Katiba Mpya leo (Jumatano, Januari 16, 2013) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba.

1 comment:

Anonymous said...

toeni maoni yenu toeni baba zangu wee lakini mkae mkijua wazanzibari wameshaamka katika ule usingizi wa kupigwa dawa za ganzi katika kufanyiwa opereshen wanachotaka ni nchi yao yenye mamlaka kamili ziyo kutiwa viraka koti kama la mchizi kila leo kurekebisha katiba ili iwe na manufaa kwenu kwao wazalilike kila leo.
wameshachoka wanataka kupu kupumuwa hawataki kuvaa koti la viraka kama machizi wanataka kuvaa koti jipya koti la muugano linawabana bwana na hawana nafasi ya kufanya mazoezi ili wakonde zaidi walivyo konda hivi sasa kwa kunyonyo. hawataki kufanya mazoezi ili wakonde ili koti liwatoshe wameshachoka wanataka kupu kupumua wacheni wapu wapumuwe.

toeni maoni lakini mnajua kwamba wazanzibari wamesha wameshaamka hawataki koti la kubana tena wala la viraka,koti jipya ndo deal