ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 26, 2013

EPIQ STARS YAACHA GUMZO MTWARA

Vijana wa Epiq Stars mwishoni mwa wiki hii wameweka historia mkoani Mtwara kwa kutoa burudani kubwa ambayo itadumu kipindi kirefu vichwani mwa wana Mtwara.
Burudani hiyo iliyofanyika katika uwanja wa Umoja zamani Nagwanda, imebaki gumzo kwa wanamtwara kwa namna vijana hao wa Epiq Stars walivyoweza kuwaimbisha na kuwachezesha mashabiki kwa zaidi ya masaa mawili bila kuchoka.
Huku mvua ikinyesha, hali ambayo kikawaida ingefanya mahudhurio ya mashabiki kuwa hafifu, lakini ilikuwa tofauti hapa Mtwara kwa mashabiki kujazana kuwaona wasanii hao.
Ikiwa ni mara ya kwanza kwa ziara hiyo kufanyika toka shindano la Epiq BSS lianze,wakazi wa Mtwara walishuhudia kwa mara ya kwanza wasanii hao walioshiriki shindano hilo mwaka jana wakizindua nyimbo zao mpya uwanjani hapo.
Huku wakiongozwa na mshindi wa shindano hilo, Walter, wasanii hao walionyesha wao ni moto wa kuotea mbali kwa uwezo wa kuimba pamoja na kumiliki jukwaa.
Burudani hiyo ambayo ilianza saa nane mchana, ilianza kwa msanii kutoka Arusha Vincent kupanda na kutoa burudani kali akifuatiwa na dada wa taarab, Husna ambaye wimbo wake wa Nawamimina unafanya vizuri kwenye vituo vya redio hapa nchini kupanda na kuwapagawisha wana Mtwara kwa uwezo mkubwa wa kumiliki jukwaa.
Kama haitoshi, msanii mwingine aliyejizolea umaarufu kwa kuimba nyimbo za asili, Nshoma aliwaonyesha wana Mtwara kuwa hata nyimbo hizo zinaweza kuwa burudani kubwa zikifanywa vizuri.
Msanii mwingine, ambaye ni ndugu wa Nshoma, Nsami, ambaye ni mkali wa kuimba nyimbo laini, aliwakonga mashabiki kwa sauti yake nzuri alipoimba wimbo wa Muongo.
kwa picha zaidi bofya read more
Ikiwa ni burudani baada ya burudani, Menina, ambaye anajua kumiliki jukwaa alipanda na kupokewa kwa shangwe kubwa kabla ya kumpisha msanii kutoka Nyumba ya vipaji, Linah ambaye aliimba nyimbo zake kali Oliver Twist na Ushafahamu.
Huku wakali kama Rich Mavoko, Barnaba na Ben Paul nao wakifanya vizuri kiasi cha kuombwa kurudia nyimbo zao, lakini vijana wa Epiq Stars nao walionyesha uwezo mkubwa katika kutoa burudani.
Kama kawaida Wababa, Norman pamoja na Menina walitoa burudani kali, ikimaliziwa na mshindi Walter, ambaye hadi anamaliza kuimba mashabiki bado walikuwa wakipiga kelele asiondoke jukwaani.
Burudani hiyo ambayo ilienda sambamba na kuadhimisha mwaka mmoja tokea club ya Maisha kuzinduliwa Mtwara, mpaka sasa imeshafika mikoa mitatu ya Dar, Mtwara pamoja 

No comments: