Marehemu Padri Evaristus Mushi
|
Mchoro huo ulisambazwa katika vyombo vya habari jana mjini hapa kutoka ofisi ya Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa na unamuonesha ‘mtu’ aliyevaa baraghashia….
Katika taarifa hiyo, Polisi ilisema kwamba mtu atakayesaidia kukamatwa kwa muuaji huyo atazawadiwa sh. 10 milioni.
Taarifa hiyo ilitaka mwananchi yeyote ambaye anamjua mtu aliyefanana na mchoro huo atoe taarifa katika kituo chochote cha polisi na iwapo atakuwa ndiye mhusika atapewa zawadi hiyo.
Kamishna Mussa hakupatikana jana kutoa maelezo zaidi juu ya hatua
hiyo, lakini Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Haji Abdallah Hanna alithibitisha kuwa taarifa hiyo imetoka Polisi.Kamanda Hanna hakuwa tayari kutoa maelezo zaidi kwa maelezo kwamba upelelezi wa suala hilo unafanywa na makao makuu ya Polisi Zanzibar.
Padre Mushi aliuawa kwa kupigwa risasi na mtu asiyejulikana Februari 17 mwaka huu wakati akienda kuongoza ibada ya Jumapili katika Kanisa la Mt. Teresia liliopo Beit el Raas nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Kuuawa kwa Padre Mushi lilikuwa tukio la tatu kubwa la kushambuliwa kwa viongozi wa dini baada ya kumwagiwa tindikali kwa Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Fadhil Soraga na kupigwa risasi Padre Ambrose Mkenda wa Kanisa Katoliki.
No comments:
Post a Comment