Tuesday, March 12, 2013

Mjadala Ughaibuni:Elimu Tanzania


Ndugu Luke
Pole sana kwa shughuli za hapa na pale na kwa kuendelea kutupatia habari kila siku bila kuchoka na zaidi kuendelea kutuunganisha kati ya watu wa hapa na wale wa nyumbani
Leo ningependa kuchukua nafasi hii kuongelea kuhusu mtizamo wangu kutokana na majadiliano wa watu wanajihita watu wa Ughaibuni katika kipengele cha elimu. Nawashukuru wote walioshiriki kwa kuchukua muda wao na kuona umuhimu wa kujadili jambo hilo. Nimefurahi zaidi kuona mitizamo ya Watanzania wanaoishi nje ya Tanzania na mimi nikiwa mmoja wao jinsi mapenzi yetu ya nchi yalivyo madogo. Nimeshtushwa na baadhi ya Watanzania hao kufikia kutoa mifano ya Tanzania na mfumo wake wa elimu wakiwa wanalinganisha na mfumo wa Kimarekani. Na nimeshutushwa na jinsi wanavyojitahidi kujiweka pembeni ya tatizo hilo wakati huo wakipenda kulijadili. Kwa kweli ndugu zangu lazima tufikie wakati tuwe na mapenzi mema na nchi yetu nikiwa na maana tusiwe wepesi kudanganyika na hapa tulipo kwani hata kama tuna uraia wa Marekani lakini walio wengi bado tu watanzania.

Katika wachangiaji wote sikusikia hata mmoja akisema kwamba alishafanya kitu katika kusaidia elimu ya Tanzania, na hapo ndipo ninaposema kweli tunajadili kwa upendo au tu kwa sababu tupo hapa.
Nilipoingia nchi hii nilikutana na Watazania wengi wenye uwezo mkubwa katika sekta mbali mbali, mara moja niligundua kwamba kuna uwezekano watanzania waliopo hapa tukawasidia wale walio nyumbani kadili ya utaalamu wepi bila hata kuomba msaada kwa Weupe. Nilianzisha mjadala wa watu kuanza kwenda nyumbani na kujitolea kama kufundisha, kutibu, kutoa utaalamu kwenye mawasiliano, na watu hao nilikutana nao ana kwa ana na nikawapa mbinu ni jinsi gani tutafanikisha, baadae wakaniambia unaonaje suala ilo ukilipeleka kanisani kwako kwani wazungu wanaweza kuwa na mvuto na suala hilo.
Sikukata tamaa, nikaanzisha mpango wa nilisoma wapi? nikiwaamashisha Watanzania wanaoishi hapa wakatafuta mawasiliano na shule zao hasa za Msingi na angalau kununua kitabu kimoja, nilitumia muda mwingi kuamashisha lakini matokeo yalikuwa madogo.

Sikukata tamaa, nilipoenda nyumbani nikakuta shule za sekondari za Kata zinasuasua, nikaja hapa na kuwa na kauli mbiu inayosema Unajua Mtoto wa Jirani yako Huko Nyumbani anasoma Wapi? Niliwafuata watanzania nikawambia kwamba kwa msaada wako wa dola ishirini za Kimarekani unaweza kubadilisha maisha ya jirani yako huko nyumbani, baadhi waliitikia lakini wengine walisema tafuta wafadhili hapo kanisani kwako.
Msistizo wangu umekuwa kama sisi tumepata bahati ya kuwa hapa na tumeona wenzetu walivyopiga hatua, si kwa msaada bali kwa tija na maarifa mchango wetu ni nini kwa watu wa nyumbani. Watu wengi tupo hapa na tunafanya kazi tatu au nne, najua ni ngumu lakini furahaa yetu itakamilika tukisikia nyumbani nao wanapiga hatua, na ni lazima tujadili mambo haya kwa vitendo badala ya kupeta mdomo tu.
Tuachane na mawazo ya kwamba tutaomba misaada wakati na sisi ambao tumepata bahati ya kuwa na senti kidogo hatupo tayari kufungua mikono yetu.
Ndio hayo yangu kwa Leo

Asante

6 comments:

Anonymous said...

Nakubaliana sana na hayo uliyosema, ningependa kuwasiliana na wewe binafsi kwani muongozo wako na wangu ni sawa. Kuna barua yangu binafsi nimetuma kwa tume unaweza kuisoma hapa

http://leadergennis.blogspot.com/

Anonymous said...

Mdau umeongea vizuri sana. Naomba tu ufahamu kuwa kuna watanzania wengi welioishi ughaibuni na kusaidia nyumbani kabla wewe hujazaliwa. Kwa hiyo siyo kuwa wewe baada ya kufika USA ndipo ukaanzisha wazo hili la kuhimiza utoaji wa misaada. Pia wewe ni nani ili kila anayesaidia nyumbani aje atoe taarifa kwako au andikwe magezitini usome? Unaposema kuwa kujadili tatizo ni lazima uwe umelitolea msaada kwanza, je hiyo ni principle, theory, law, or you own opinion? Badala ya kulalamikia dola 20 za wabeba box, umewahi kuwashirikisha mafisadi/wala rushwa wenye utajiri wa kutisha mawazo yako kule nyumbani? Waliokwambia uende ukaombe msaada kanisani walijua kama unamatatizo. Anayesaidiwa ni mgonjwa, mlemavu na mzee. Haiwezekana Tanzania inakuwa na maajabu makubwa matatu kati ya saba barani Afrika na bado hadi leo inakuwa ombaomba. Ukipata nafasi nenda Rwanda kawaulize nini walifanya baada ya genicide. wanaongoza kwa kila kitu Afrika mashariki waati hawana mlima Kilimanjaro, Tanzanite, diamond, gold, Ngorongoro, Mikumi, Serengeti wala gesi asilia.

Anonymous said...

Mdau ni vizuri ungeuliza kwanza kuwa unapoandika article kama hii ni busara kuweka jina lako. Unapoacha kuandika jina wasomaji wanaweza kujiuliza maswali mengi dhidi yako. Kama una nia nzuri na nchi yako, pia una uchungu na elimu, kwanini unajificha?

Anonymous said...

Mimi nami nakuunga mkono ktk hili jambo. Tatizo kubwa hapa kwa wachangiaji ni hili, hawana uchungu na suala zima na pia aliyeandaa mdahalo ule hakuzingatia kwamba ni akina nani wanafaa kutoa hoja. Wataalamu wa elimu mjitokeze na kulijadili jambo hili kiutalaamu wa hali ya juu. Hili si jambo la kujadili kwenye baa, send off, kanisani nk.

Anonymous said...

Watu tulio huku inabidi tufikirie kwa ukubwa zaidi badala ya kutumia mbinu za kizamani. Tatizo kubwa Tanzania sio pesa badi ni mpango. Watanzania wapo tayari kusaidia kama kuna mpango mzuri wa kusaidia Mfano. Serikali ikiweka mpango wa vijana wa vyuo kufundisha kwa miezi sita kwenye shule za sekondari hasa kwa wale waliopewa mikopo na serikali halafu kukawa na Kamati binafsi ya kuchangisha pesa kwenye kampuni na watu binafsi kuhakikisha hao wanavyuo wanapesa ya matumizi wanapoenda kufundisha Watanzania wengi wangechangia hata sisi wa huku. Sababu kubwa ya kuchangia ni kwamba tunaweza kupima maendeleo ya hiyo misaada. Hatutafanikiwa kama kila mtu anatoa $10, $20 na huna uhakika kama inaenda kwa mwanafunzi au mke wa pili!!. Watanzania wanapenda kusaidia lakini hakuna watu wa kufanya organization kama hizi. Viongozi wastaafu wa nchi za wenzetu wanafanya vitu kama hivi angalia Clinton na Carter.

Anonymous said...

1. Anayedai kuwashawish wengine watoe pesa kusaidia elimu nyumbani, anajuaje hiyo pesa haitaishia mikoni mwa wala rushwa kujengea majumba ya kifahari? Ni kweli huyu menzetu ndiye hana uchungu na nchi yetu.

2. Kuna wengi wamesaidia katika njia mbali mbali kinyume na ya kwako. Kwa vile njia zao ni tofauti na yako haina maana hawana uchungu na nchi yao.

3. Hili swala limemgusa kila m-Tanzania. Hivyo naashauri aliyeandaa mjadala huu, atembelee sehemu zingine kuwapa wa-Tanzania fursa ya kujadiliana kama alivyofanya kwa wana DMV.

Good job, Mr. DJ Luke.