Ziara hiyo ambayo ilijumuisha wasanii wote wa nyumba ya vipaji kama Ditto, Mwasiti, Barnaba, Amini, Linah, Makomando, Ali Nipishe, Mataluma na The Trio, iliwapa fursa watoto kuzungumza na wanamuziki hao wanaowapenda pamoja na kupata burudani ya muziki kutoka kwao.
Barnaba na Linah wakiwaimbia watoto.
Wakizungumza hospitalini hapo baada ya kuwaona wagonjwa hao, msanii Ditto alisema wameamua kutoa muda wao ili kuwafariji watoto hao kama mchango wao kwa jamii.
Linah akiimba na mtoto.
Nao watoto wanaopata matibabu hospitalini hapo walipongeza wasanii wa THT kwa kuwakumbuka, huku wakiomba wasanii wengine na jamii isiwasahau.
Muki, Mwasiti na Linah wakiimba.
Wasanii wa THT wakiwa na picha ya pamoja na watoto.
No comments:
Post a Comment