BANGO lililombeba ujumba wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya utumwa na biashara ya utumwa, maadhimisho ambayo yalifikie kilele Marchi 25 hapa Umoja wa Mataifa.
Professa Ali Mazrui, Mwanazuoni maarufu akisaidiwa kuketi kabla ya kuzungumza katika siku hii ya maadhimisho ya kumbukumbu ya utumwa na biashara ya utumwa
Professa Mazrui akizungumza ambapo pamoja na mambo mengine alielezea histotia ya utumwa na biashara ya utumwa pamoja na harakati mbalimbali zilizopelekea kukomeshwa kwa biashara hiyo. pamoja na kusisitiza haja na umuhimu wa kuendelea kuwaenzi waathirika wa ukatili huo, alitaka pia kuenzi yale mema ambayo baadhi yake ni matokeo ya historia hiyo ya Utumwa, Professa Mazrui alikuwa mzungumzaji mkuu katika maadhimisho haya ambayo hufanyika Machi 25 ya kila mwaka.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, ambapo pamoja na mambo mengine alisisitiza Jumuiya ya Kimataifa kuendelea kupambana na utumwa unaoendelea hivi sasa kila pembe ya dunia.
hii ni Nakala Halisi ya Tangazo la Ukombozi wa Watumwa ( Emancipation Proclamation) iliyotiwa sahihi mwaka 1864 na Rais Abraham Lincoln na aliyekuwa Waziri wake wa Mambo ya Nje wakati huo, Bw. William H. Seward. Nakala hii ambayo ilioneshwa pamoja na maonesho mengine yaliyohusu utumwa na biashara ya utumwa ni kati ya nakala 48 ambazo Rais Lincoln alizisaini, na zikauzwa kwa dola kumi kila moja kati ya juni 7 hadi 29, 1864 huko Philadelphia kwa lengo la kupata fedha za kuwasaidia maveterani wa vita. inasemekana ni kati ya nakala hizo 48 ni 26 tu ndiyo bado zipo moja ikiwa ni hii ambayo ilipatikana kwa hisani ya Bw. Lawrance
Na Mwandishi Maalum
Mwanazuoni Maarufu Professa Ali Mazrui, amesema, wakati jumuiya ya kimataifa inapokumbuka, ukatili, ubaguzi, unyanyasaji
na kila aina ya uovu aliotendewa mtu mweusi kupitia utumwa na biashara ya
utumwa, yapo mambo mazuri ambayo kwayo
anasema yapashwa kuenziwa.
Alikuwa akizungumza wakati wa siku ya Kimataifa ya kumbukumbu ya
Utumwa na Biashara ya Utumwa, ambayo imeadhimishwa jana ( jumatatu ) hapa
Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Mwanazuoni huyu maarufu na mtaalamu aliyebobea katika Historia ya Bara
la Afrika na anayeheshika sana, alikuwa mzungumzaji mkuu katika siku hii ambayo
miaka sita iliyopita, Baraza Kuu la
Umoja wa mataifa liliitenga rasmi Machi
25 ya kila mwaka kama siku maalum ya kuwakumbuka na kuwaenzi waathirika wa ukatili huu uliofanyika zaidi ya miaka 400 iliyopita.
“ Leo hii tunapowaenzi na kuwakumbuka wahanga wa
utumwa na biashara ya utumwa, na
historia nzima ya harakati zilizopelekea
kukomeshwa kwa biashara hii, lazima pia tujifunze kutoka na histollia ile kwa kutambua na kuenzi mema ambayo baadhi yake
yanatokana na historia hiyo.”
akasema Professa Mazrui.
Kwa habari na picha zaidi bofya read more
Kwa mtizamo
wake, anayataja baadhi ya mambo hayo
kuwa ni pamoja urithi ulioachwa na Martin Luther King ( jr), mambo mazuri
yaliyofanywa na Rais Mstaafu wa Afrika
ya Kusini Mzee Nelson Mandela, Marekani kuwa na Rais wa kwanza mwenye asili ya
Afrika, Katisa Katoliki kuwa na Papa
wa Kwanza kutoka Amerika ya Latini,
wanawake kuendesha harakati za kujiwezesha
na kujikomboa kiuchumi na kuibuka kwa mataifa mapya yanayokua kiuchumi duniani.
Professa Mazrui
ambaye alionekana wazi kuelemewa na utu uzima, licha ya kuelezea kwa kina
harakati mbalimbali zilizochangia kwa namna moja ama nyingine kukomeshwa
kwa utumwa na biashara ya utumwa,
alitumia fursa ya siku hii, kumkumbuka na kumuenzi Chinua Achebe aliyefariki
wiki iliyopita. Professa akamuelezea
Chinua Achebe kama mmoja ya watu mahiri na mashuhuri ambaye kwa kutumia
kalamu yake alipigania utu, heshima , hadhi na utamaduni mwa mtu mweusi.
Akasema dunia na hasa Afrika imempoteza
mtu muhimu sana.
Awali akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, aliitaka Jumuia ya Kimataifa kuelekeza nguvu zake katika kuukabili utumwa
na biashara mpya ya utumwa inayoendelea kushika kasi hivi katika kila pembe ya dunia.
Akautaja utumwa huo kuwa ni pamoja na biashara ya utumwa wa ngono, ajira za watoto
wadogo, biashara ya usafirishaji wa
binadamu na matumizi ya watoto wadogo
katika vita.
Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kumbukumbu ya utumwa na biashara ya utumwa yalitanguliwa na shughuli mbalimbali zilizofanyika
kwa wiki zima.
Baadhi ya shughuli hizo zilikuwa ni pamoja na mijadala ya kisomi
iliyowashirikisha watafiti na wataalamu wa historia ya utumwa na ukomeshaji wake, mijadala iliyowashirikisha wanafunzi kutoka
mabara mbalimbali, mijadala ya Asasi
zisizo za Kiraia na maonesho ya muziki na Nakala Halisi
ya Tamko la Ukombozi wa Watumwa, nakala hii ni
kati ya nakala chake zisizozidi 48
ambazo Rais Abraham Lincoln na Waziri
wake wa Mambo ya Nje Bw. William H. Seward walitia sahihi mwaka 1864.Benson
Steel Pulse mwanamuziki wa kimataifa wa muziki wa Rock ambaye amekuwa akitumia kipaji chake kuelimisha na kuhamasisha kuhusu ukatili anaotendewa mtu mweusi, Bw. Steel Pulse alikuwa kati ya wanamuziki waliotumbuiza katika tamasha maalum la kuwaenzi waathirika wa utumwa na biashara ya utumwa.
Omi Mwanamziki wa Kizadi kipya wa Muziki wa Jazi, kutoka Afrika ya Mashariki naye aliwapagaisha washiriki wa tamasha la muziki kwa vibao vyake murua vilivyokuwa na radha ya muziki wa Jazi kwa kuchanganya na midundo ya kibantu ambayo mwenyewe anaita " New African Jazz" Somi alitambuliwa kama Baba yake ni Muganda na Mama yake Mnyarwanda
Kikundi cha Utamduni kutoka nchini Cameroon wakitumbuiza wakati wa Tamasha maalum la Muziki kuadhimisha kumbukumbu ya waathirika wa utumwa
hawa pia wanatoka Cameroon wakiburudisha
Biashara ya utumwa haikufanyika kupitia bahari ya Atlantik peke yake bali hata Bahari ya Hindi kwa watumwa waliotoka Afrika ya Mashariki, Balozi za Tanzania na Kenya katika Umoja wa Mataifa, zilifanya onesho la Khanga zilizobeba ujumbe mbalimbali, kama sehemu ya kuenzi utamaduni mwa mwafrika na wakati huo huo kukitangaza kiswahili, washiriki wa tamasha la utamaduni ambalo lilikukwenda samabamba na vyakula vya asili ya afrika walifurahia sana tafsri ya kila ujumbe uliokuwa katika khanga hizo.
wanamuziki hawa waliokuwa pamoja na Steel Pulse wakicharaza magitaa yao kwa uhodari mkubwa pali kuwa hapatoshi
Wanamuziki hawa walisindikiza mwanamziki mwigine kutoka Afrika ya Magharibi, Benyoro ambay naye alikuwa kivutio kikubwa
Benyoro akifanya vitu vyake
Mwanamuzi mwingine maarufu kwa kulicharaza gitaa na ambaye pia ni Mjumbe Maalum wa UNESCO katika mradi wa kutafiti njia za Biashara ya Utumwa akiimbia kwa hisia kali wakati wa Tamasha la Muziki, Marcus Miller amewahi kushinda mara mbili Tuzo ya Grammy katika midundo ya American Jazz
No comments:
Post a Comment