Tuesday, March 26, 2013

WABUNGE ZITTO, AZAN NA WABUNGE WENGINE WAMALIZA MAFUNZO YAO YA JKT KAMBI YA MGAMBO 835KJ LEO


Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi mbunge wa viti maalum Ester Bulaya leo katika kambi ya RUVU JKT.Rais Kikwete amefunga rasmi mafunzi hayo leo yaliyofanyika kwa wiki tatu.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe pamoja na Wabunge wenzake kadhaa vijana leo wamemaliza rasmi mafunzo yao ya awali ya JKT katika kambi ya Mgambo 835KJ kilichopo Mkoani Tanga.

Pichani juu ni Zitto Kabwe akijiandaa kwenda katika gwaride la mwisho na picha chini akiwa shambani pamoja na Mbunge mwenzake Iddi Azan, Abdallah haji, Raya Ibrahim na Antony Mbassa kambi ya Mgambo 835KJ.
Aidha Zitto Kabwe amesema anafuraha iliyo pitiliza kumaliza mafunzo hayo na ameweka historia ya kubwa katika maisha yake hii leo.

Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya pamoja na wenzao wakila kiapo wakati wa kuhitimu mafunzo ya muda mfupi yaliyofanyika katika kambi ya jeshi la Kujenga Taifa Ruvu JKT huko kibaha Mkoani Pwani leo.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi kutoka kwa kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Muhingo Rweyemamu wakati wakimaliza mafunzo ya JKT, katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Kwa picha zaidi bofya read more
wakwanza katika mstari wa kushoto ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe anayefuata ni Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani, wakiwa kwenye Paredi ya kumaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT Kikosi cha 835 Mgambo JKT kambi iliyopo katika Kata ya Mgambo ilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
wakwanza kushoto ni Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, ZItto Kabwe, wakihitimu mafunzo ya JKT katika kambi ya 835 Mgambo JKT iliyopo Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani, akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Biharamulo, Dk Athanas Mbassa, akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga. picha na Hussein Semdoe.
Mbunge wa Kiwani Pemba, Abdallah Haji Ali, , akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, akiapa mbele ya kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Muhingo Rweyemamu, hayupo pichani, wakati wakimaliza mafunzo ya JKT, katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge Viti maalum Raya Khamis , akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni.
Baadhi ya Wabunge walikuwa wakichukua mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.

No comments: