Tuesday, March 12, 2013

Wanafunzi wa skuli ya Kusini waelekea Sweden

Wanafunzi wa skuli ya Kusini wakiwa nje ya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar kabla ya kuondoka kuelekea Sweden kwa ziara ya kimasomo. Skuli ya kusini iliyoko Makunduchi imeanzisha uhusiano na Skuli iitwayo Sundsvall ya Sweden.
Katika uhusiano huo ulioanza mwaka jana wanafunzi pamoja na walimu wa Sundsvall wameshawatembelea wenziwao Skuli ya Kusini mara mbili. Katika uhusiano huu walimu wa skuli ya Kusini watajifunza mbinu za kisasa za ufundishaji kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano ICT.
 Skuli za Makunduchi zimo katika harakati za kutafuta njia bora za ufundishaji kufuatia ufaulu mbaya katika mitihani ya taifa uliozikumba skuli nyingi hivi karibuni hapa nchini.
 Katika picha wa kwanza kutoka kushoto ni mwalimu Juma Ali Simai ambaye ni mratibu wa safari hiyo, na wa kwanza kutoka kulia ni Mwalimu Mkuu ndugu Shamsi Ameir.
Uhusiano huu ulioanzishwa ni kutokana na jitihada za walimu wenyewe wakisaidiwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Mzuri Kaja (Mzuri Kaja Development Society - www.mzuri-kaja.or.tz)

Zanzi News

2 comments:

Anonymous said...

mkifika huko msome msifanye maskhara na wala msikubatiye mkawa libukeni utamaduni wa watu kuweni na utamaduni wenu na shikeni dini yenu msiache kusali hata siku mmoja mmesikia ushauri wa bure kutoka marekani.

Anonymous said...

jamani nakuombeni msome kwa bidi na msisahau kilichokupelekeni huko na msisahau mila na tamaduni na dini zenu please kila la kheri

dini zenu msipuze jamani ni muhimu sana please