ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, April 21, 2013

Majambazi yaua, yapora mamilioni

Arusha. Mtu mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi na wengine wawili wamejeruhiwa, akiwamo askari polisi, baada ya majambazi kuvamia gari lililokuwa limebeba Sh58 milioni zilizokuwa zinapelekwa benki.
Tukio hilo lilitokea jana saa 5:30 asubuhi katika eneo la Idara ya Maji, katikati ya Jiji la Arusha na kuzua tafrani ya aina yake, baada ya majambazi hao kupiga risasi ovyo hewani kabla ya kupora kiasi hicho cha fedha.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Ibrahim Kilongo alithibitisha kutokea kwa mauaji na uporaji huo wa fedha za Kampuni
ya Mafuta ya Panone.
Kamanda Kilongo, alisema majambazi hayo yakiwa na pikipiki, yalivamia gari lililokuwa likiendeshwa na Moses Masania, akiwa na wahasibu wawili Hapiness Ndasai na Jacline Dastin wa kampuni hiyo.
Alisema majambazi hayo yaliyokuwa matatu, yakitumia pikipiki, yalizuia gari hilo kwa mbele eneo la Idara ya Maji na kuvunja kioo cha mbele cha gari na kisha kumpiga risasi Masania ambaye alifariki papo hapo. ya Mafuta ya Panone inayomilikiwa na Patrick Olomi. Kamanda Kilongo, alisema majambazi hao wakiwa na pikipiki, walivamia gari lililokuwa likiendeshwa na Moses Masania, akiwa na wahasibu wawili Hapiness Ndasai na Jackline Dastin wa kampuni hiyo.
Alisema majambazi hao waliokuwa watatu, wakitumia pikipiki, walilizuia gari hilo kwa mbele eneo la Idara ya Maji na kuvunja kioo cha mbele cha gari na kisha kumpiga risasi Masania ambaye alifariki papohapo.
Kamanda Kilongo alisema katika vurugu hizo za uporaji, majambazi hao pia walimjeruhi kwa risasi Hapiness na askari polisi Koplo Kudura aliyekuwa njiani katika shughuli zake.
“Wote walipata majeraha kidogo, na polisi aliyepigwa risasi mguuni alitibiwa na anaendelea vizuri,” alisema Kamanda Kilongo. Alisema katika tukio hilo majambazi hao walifanikiwa kutoweka na fedha Sh58 milioni zilizokuwa zinapelekwa benki.
Tukio hili limekuja wakati matukio ya ujambazi yameanza kurejea Arusha, kwani hivi karibuni majambazi walimuua kwa risasi mfanyabiashara wa madini na kutoweka na madini aliyokuwa nayo.
Kamanda Kilongo ametoa wito kwa wafanyabiashara wanaobeba fedha nyingi kupeleka benki, watoe taarifa ya kuomba msaada kwa polisi.
Hata hivyo, alisema hadi kufikia jana jioni msako wa kuwakamata majambazi hao, ulikuwa unaendelea.
Mwananchi

No comments: