Thursday, May 16, 2013

CCM – CALIFORNIA WAANDA NYAMA CHOMA “MEMORIAL WEEKEND”

Chama Cha Mapinduzi  (CCM) - California kinawakaribisha watanzania  na mataifa mengine waishio California bila kubagua itikikadi za kisiasa katika  siku ya Nyama Choma – (BBQ) itakayofanyika siku  ya “memorial weekend”  tarehe 25 mwezi  wa tano, mwaka 2013. Kuanzia saa sita mchana mpaka kumi na mbili jioni. Anuwani ya shughuli ni 
17600 Lake Chabot Rd  Castro Valley, CA 94546
Baada ya nyama choma kutakuwa na burudani ya muziki itakayoanza saa tatu na nusu ya usiku mpaka saa nane asubuhi katika ukumbi wa  Café Randevu ulioko mjini Oakland. Anuwani  ya ukumbi  wa muziki ni 2430 Broadway  Oakland, CA 94612
Kiingilio cha muziki kitakuwa ni $10.00  tuu . DJ TOM, mtanzania aliyebobea safu za miziki  na hasa ule  wa kinyumbani atakuwa  akiwakata kiu na kuwarusha roho na nyimbo za bongo flava  kwa  vibayo vipya na vya zamani.
Kwa maelezo wasiliana na:-

Jospehine M.  – 510-484-5085
Mwenyekiti CCM - California

Erick B.  – 510-520-5995
Katibu CCM - California

KARIBUNI WOTE

2 comments:

Anonymous said...

Jamani kuna watu wanapenda CCM ! Mpaka kuandaa nyama choma. Hongereni wakeretwa na endeleeni na moyo huo huo.

Anonymous said...

Kidumu chama cha mapinduzi. Juhudi hizi za kuwa karibu na masuala ya nchi yetu kwa kutumia asasi zilizoararishwa kama vyama tuziunge mkono. Nia ni njema kabisa na nawapongeza ccm kwa kuwa mkakati huo wa kuwachangamsha watu na nyama choma. Vyana au siasa si ugomvi bali changamoto za kuuafuta majibu na dawa ya matatizo ya nchi yetu. Lakini pia kushirikiana kwa upendo.