Serikali imetoa sababu za kuzuia uvuvi wa samaki aina ya kamba kuwa ni uchache wa samaki hao katika maeneo ya ukanda wa Tanzania.
Hayo yalielezwa jana na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Benedict Ole Nangoro wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kilwa, Multaza Mangugu (Kilwa Kaskazini-CCM) ambaye alitaka kujua ni sababu zipi zilizopelekea Serikali kuzuia samaki hao kuvuliwa kwa kipindi cha miaka mitatu sasa.
Mbunge huyo alisema kuwa maisha ya samaki hao ni miezi 9 katika uhai wao tangu kuzaliwa hadi kufa lakini Serikali imezuia wasivuliwe kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.
Awali katika swali la msingi,Conchesta Rwamlaza(Viti Maalumu- Chadema),alihoji Serikali ina mpango gani wa kuwapa nguvu wafugaji wa samaki katika mabwawa mkoani Kagera.
Naibu Waziri alisema, Serikali inatambua umuhimu wa wafugaji wa samaki katika maeneo ya Mkoa wa Kagera na tayari imeshawapeleka wataalamu wawili mahsusi katika ufugaji wa samaki ambao watatoa elimu kwa wafugaji wa samaki.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment