Wednesday, June 12, 2013

KIBARUA CHA ASKARI WA KIKE ALIYEPIGA PICHA ZA UTUPU CHAOTA NYASI

WP Amisa
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemfukuza kazi askari wake wa kike, WP Amisa, aliyekuwa akifanya kazi kituo cha Polisi Magomeni kutokana na utovu wa nidhamu.
Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna wa Polisi Suleiman Kova amesema, Amisa amefukuzwa kazi kwa kuwa amekiuka maadili ya Jeshi hilo kwa kitendo chake cha kupiga picha za utupu zilizoonekana katika mitandao.

4 comments:

Anonymous said...

Hapo naunga mkono kabisa sababu Police lazima wachukuliwe kiwango cha juu sana kuliko watu wa kawaida sasa kama utaenda kupiga picha za utupu uweke kwenye mitandao halafu utegemee kuendelea na kazi ni kitu kisicho wezekana kabisaaa. Nidhamu ni muhimu sana wewe kama police. Wawafukuze kazi na wafanya magendo woote na wala rushwa woote hapo nitafurahi sana. Haya bi dada katafute kazi kwenye porn industry faster. Goodluck.

Anonymous said...

wabaya wake wamemchomeya mbona hii kazi hata ma mp wanafanya bongo kila aliye mke au mume wa mtu usisikiye ni kiwembe kwenda mbele sema bado siko zao arubaini kufumwa tu wanamuonea bongo ndo fashio hilo hata si jambo la kushanga mshangae mlio majuu msiojua yanayojiri huku

Anonymous said...

ni vyema jeshi la polisi bila lisingepupa kumfukuza kazi kabla ya kuchunguza mazingira ya kupiga kwake picha hizo... yawezekana kapiga na mpenzi wake wakiwa chumbani baadaye mpenzi huyo kwa ulimbukeni au hasira za kukataliwa akaamua kuzituma mtandaoni ilikumkomoa... siungi mkono uamuzi wa kumuachisha kazi kama ulivyochukuliwa.

Anonymous said...

Wamemuonea,mdau wa 4.38am umeongea kweli jamaa kapigwa chini kaamua kuharibu Mungu atakupa kaxi nyingine dada.