ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 5, 2013

Dual Citizenship na Rasimu ya Katiba Mpya ipitie toa maoni yako

SURA YA TANO
URAIA KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO
54.-(1) Mtu ambaye,kablaya Katiba hii kuanza kutumika, ni raia wa Jamhuri ya Muungano ataendelea kuwa raia wa Tanzania.
(2) Uraia wa Jamhuri ya Muungano ni wa aina mbili na utapatikana kwa njia ya kuzaliwa au kujiandikisha.
55.-(1) Kila mtu anayezaliwa Tanzania Bara au Zanzibar atakuwa raia wa Jamhuri ya Muungano iwapo, wakati wa tarehe ya kuzaliwa, mama au baba yake ni au alikuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, mtu aliyezaliwa nje ya Tanzania atakuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzaliwa kuanzia tarehe ya kuzaliwa kwake ikiwa wazazi wake au mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa Jamhuri ya Muungano.
(3) Endapo mmoja kati ya wazazi alifariki kabla ya mtu huyo kuzaliwa, uraia wa mzazi huyo wakati wa kifo chake unatumika, kwa madhumuni ya kutambua uraia wa mtu huyo aliyezaliwa baada ya mzazi aliyefariki kama kwamba mzazi huyo alikuwa anaishi hadi kuzaliwa kwa mtu huyo.
(4) Mtoto mwenye umri chini ya miaka saba akikutwa ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Muunganokatika mazingira ambayo wazazi wake hawajulikani, atahesabika kuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuzaliwa.
(5) Mtoto aliye na umri wa chini ya miaka kumi na nane ambaye wazazi wake sio raia wa Tanzania, akiasiliwa na raia wa Jamhuri ya Muungano, kwa kuasiliwa kwake huko, kutawezesha mtoto huyo kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa kujiandikisha.
56.-(1) Mara baada ya kuanza kutumika kwa Katiba hii, mtu ambaye amekuwa mkazi wa Tanzania Bara au Zanzibar kwa muda uliowekwa na sheria inayotumika Tanzania Bara au Zanzibar, na ambaye ametimiza masharti yote ya sheria ya Bunge la Tanzania Bara au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, anaweza kuomba kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Mtu aliyefunga ndoa na raia wa Jamhuri ya Muunganoanaweza kutuma maombi ya kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(3)Endapo ndoa iliyorejewa katika Ibara ndogo ya (2) itavunjika, kama mtu huyo hakuukana uraia wake, ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(4) Mtoto aliyezaliwa katika ndoa iliyorejewa katika Ibara ndogo ya (2), ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa kama ataukana uraia huo au ataomba na kupata uraia wa nchi nyingine.
(5) Bunge litatunga sheria, pamoja na mambo mengine, kusimamia masuala yanayohusu uraia wa Jamhuri ya Muungano

Mdau,
ATL, GA

toa maoni yako hapa Nimepitia rasimu ya katiba mpya na kugundua kwamba haisemi chochote juu ya uraia pacha. Naambatanisha kipengele cha Uraia kilichomo kwenye Rasimu ya Katiba Mpya inayopatikana kwa kufuata link hii:
http://www.jukwaalakatibatz.com/images/downloads/RASIMU.pdf

1 comment:

Anonymous said...

I did'nt see any thing in relation to dual citizenship...are these people drunk or just dumb..???