Bert Trautmann
Dar es Salaam. Kocha wa zamani wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) na kipa wa Manchester City, Bert Trautmann (89) amefariki dunia, nyumbani kwake La Losa, near Valencia, nchini Hispania.
Kifo cha kocha huyo wa Stars mwanzoni mwa miaka ya 60, kimethibitishwa na msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura kupitia taarifa aliyotuma kwenye vyombo vya habari jana.
Mapema mwaka huu, kipa huyo alikumbwa na matatizo makubwa ya shinikizo la damu mara mbili tofauti kabla madaktari kuokoa maisha yake.
Kipa huyo askari mateka wa Ujerumani aliyekuja kuweka makazi yake Uingereza, atakumbukwa kwa mchango mkubwa aliotoa na kuiwezesha Man City kutwaa taji la FA mwaka 1956 pamoja na kwamba alicheza dakika 17 za mwisho akiwa amevunjika shingo.
Mke wa Trautmann, alithibitisha kifo cha mume wake, ambapo Chama cha Soka Ujerumani kupitia Rais Wolfgang Niersbach kimetuma salamu za rambirambi.
Niersbach alisema: “Bert Trautmann alikuwa mwanamichezo shujaa.
Alikwenda Uingereza kama askari, lakini alikuja kuwa shujaa wa mchezo wa soka.”
Aliongeza: “Mazuri aliyofanya yatabaki kuwa kumbukumbu isiyofutika milele yote na kuingia kwenye vitabu vya kumbukumbu ya mchezo wa soka.
Trautmann alikuwa askari kijana wa miavuli wakati wa utawala wa Adolf Hitler Youth na alikuwa mstari wa mbele katika vita ya Nazi Ujerumani wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Alikamatwa na vikosi vya muungano mwishoni mwa vita na kupelekwa gerezani mjini, Lancashire.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment