Wednesday, July 17, 2013

MDADA ASAHAU WATOTO KWENYE GARI KISA SHOW YA LIL WAYNE


Brittany Harris aliswekwa ndani siku ya Jumapili July 14, 2013 kwa kuwasahau watoto wake wawili kwenye gari ili aweze kuhudhuria onesho la mwanamuziki wa hip hop wa Marekani, Lil Wayne lililokua linafanyika kwenye mji wa West Palm Beach, jimbo la Florida.

Watoto wake wenye umri wa mika 3 na 5 walikutwa na mfanyakazi aliyekua kitengo cha maegesho ya magari kwenye onesho hilo akiwakuta watoto hao  wamezungukwa na maelfu ya watazamaji wengine waliokuwepo kumuangalia Lil Wayne. Mfanyakazi huyo aliwakabidhi watoto hao kwa mamlaka husika.

Brittany Harris, 25, alikubali makosa yake na ameachiwa kwa dhamana ya $6,000 huku watoto wake wakichukuliwa na mamlaka inayoshughulikia maswala ya watoto na familia ya jimbo la Florida.

Siku hii ya July 14, 2013 ilikua ni onesho la tano Maneshosho ya Lili Wayne yanayoendelea nchi nzima, Maonesho haya yamebeba jina la American's Most Wanted Tour na wasanii wengine walioambatana na Lil Wayne ni T.I, 2 Chariz na G-Easy.

No comments: