Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima (kulia) akiruka kukwepa kwanja la beki wa Mtibwa Sugar, Hassan Ramadan (katikati) wakati wa mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu kujiandaa na Ligi Kuu ya Tanzania Bara inayotarajia kuanza Agosti, 24, mwaka huu, ambapo pia ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Hisani katia ya Yanga na Azam, unaotarajia kupigwa mwezi huu.
Katika mchezo huo Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 3-1, bao la kwanza la likifungwa na Said Bahanuzi katika dakika ya 26, bao la pili likifungwa na Jerry Tegete, kwa mkwaju wa penati baada ya yeye mwenyewe kuangushwa katika eneo la hatari katika dakika ya 81 huku hitimisho la mabao hayo likihitimishwa na Hussein Javu, katika dakika ya 87.
Na bao la kufutia machozi la Mtibwa Sugar, lilifungwa na Shaaban Kisiga, kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 57.
Mshambuliaji wa Yanga, Said Bahanuzi (katikati) akijaribu kuwatoka mabeki wa Mtibwa Sugar, wakati wa mchezo huo, uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo jioni.
Kipa wa Mtibwa Sugar, akiokoa moja ya hatari langoni kwake.
Mshambuliaji wa Yanga Jerry Tegete (kulia) akimlamba chenga kipa wa Mtibwa Sugar, Hussein Sharif, wakati wa mchezo huo.
Kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohamed, akijaribu kuokoa mkwaju wa penati, uliotiwa nyavuni na Jerry Tegete.
Wachezaji wa Mtibwa wakipita kuwasalimia wachezaji wa Yanga, kabla ya kuanza kwa mtanange huo.
Kikosi cha Yanga kilichoanza.
Kikosi cha Mtibwa kilichoanza.
Benchi la wachezaji wa akiba la Yanga.
Benchi la viongozi na wachezaji wa akiba wa Mtibwa.
Baadhi ya wachezaji wa Yanga, Mrisho Ngassa na Simon Msuva, wakiwa jukwaani wakifuatilia mtanange huo.
No comments:
Post a Comment