Mtoto Ashura Mustapha anayesumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi.
Na Martha Mboma
MTOTO Ashura Mustapha (7) mkazi wa Mwandege, wilayani Mkuranga, Pwani anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi tangu akiwa na mwaka mmoja.
Mtoto Ashura Mustapha akiwa na baba yake Mustapha Makombe.
Akizungumza na mwandishi wetu, baba mzazi wa mtoto huyo, Mustapha Makombe alisema: “Mwanangu anateseka sana jamani, ugonjwa ulianza kama malengelenge akiwa na umri wa mwaka mmoja tukawa tunakwenda hospitali ndogondogo lakini baadaye tukaamua kumpeleka Muhimbili ambapo tulipewa barua ya kutuelekeza kwenda CCBRT, kule ndipo wakagundua mwanangu ana kansa ya ngozi steji ya nne.
“Baada ya kuhangaika katika hospitali nyingi bila mafanikio, nikaamua kwenda Hospitali ya Regency (Dar) kuomba msaada wa kwenda kutibiwa India.
“Pale waliniambia nichangie shilingi milioni moja na laki tano kwa ajili ya tiketi na viza ili mwanangu akatibiwe India, hizo hela mimi sina. Naomba Watanzania mnisaidie hata kwa fedha za mitandao kwa namba 0769 517765 na 0715 424697 ili niweze kumpeleka mwanangu India akatibiwe,” alisema baba mzazi.
9 comments:
eh Mungu mnusuru motto wako.mponye na mbariki...Amen! jamani kila ukiamka mshukuru Mungu kwa kila jambo.kuna watu duniani wanashida kuliko zako.
oh jamani tumsaidie huyu baba ana machungu sana moyoni akimwona mwanae kutoa ni moyo. Million 1.5 sio hela nyingi tumsaidie please please
Kweli jamani mtoto huyu wa kusaidiwa. tufanye kusaidia?
Hakika tumsaidieni huyu mtoto na msaada wetu usiishie hapo. Tuendelee kuwasukuma wanasiasa waboreshe sera za afya ili jambo kama hili lisitokee tena.
Kila mwaka tunasikia uchumi unakua kwa asilimia 6%, huo uchumi unamsaidiaje mtanzania kama huyu?
Hakika hii ni dharura na hii kesi ipelekwe Bungeni na watawala wa nchi waone kiasi gani mtanzania wa wastani hanufaiki na siasa zao.
Wako wapi wanaojiita mabuzi, wanahonga wanawake pesa kama njugu, jamani Watanzania ina maana wizara ya afya imeshindwa kumsponser huyi, madhirika ya simu, na mapombe mnatoa mamilioni kufadhili anasa mashimdano ya ujinga mnashindwa kumuhudumia huyu mtoto..eeh mungu muonyeshe njiaja wako
Naomba Mungu awape nguvu, na amponye mwanao. Mateso aliyoyapata kwa muda mrefu Mungu ayaondoe. Amen
Huyu kijana kwa nini asipelekwe India etc, hizo hela zetu mbona zinatumiwa na vigogo tu kwenda nje. They are paid very highly and we even pay for their medical expensed in foreign countries. can the government help this kid?? Whats the criteria used for sending politicians and bureacrats abroad and this poor kid big NO?
Kwa jina la yesu pokea uponyaji wa mwili mzima sasa pale ulipo. Mungu awatie nguvu na kuwavusha hapa. Natuma mchango kwa mpesa kwenye namba uliyotoa.
Mafisadi yanatibiwa nje, sisi masikini ni Ilala au Mwananyamala, huo usawa uko wapi? Lazima tuamke sisi wabongo, bado tuko waoga mno kufuatilia haki zetu!!
Post a Comment