ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 22, 2013

BRADLEY MWANAUME WA JESHI LA KIMAREKANI ALIYE TOA SIRI ZA JESHI HILO KUPITIA INTERNET KUKWEPA KUFUNGWA JELA YA KIJESHI YA WANAUME KWA SHARTI LA KUBADIRISHWA JINSIA

Bradley Manning 
Mwanajeshi huyu wa Marekani amehukumiwa kifungo cha miaka 35 jela na mahakama ya kijeshi hiliyopo Fort Meade Md. Lakini masharti aliyo yatoa kabla ya kuanza kutumikia kifungo hicho ni kubadilishwa jinsia kwa kupandikizwa hormone za kike ni aitwe Chelsea Manning, baada ya Bradley jina lake la sasa. Manning alitoa siri za jeshi la Marekani kupitia internet akiwa Afghanistan katika kituo cha kijeshi cha Marekani. Kwaiyo kwa kosa hilo serikali ya Marekani kupitia mahakama ya kijeshi ukumu yake ni maximum ni miaka 90 jela na  baada ya kupitia vipengile vya hapa na pale ameangukia puwa na kupewa kifungo cha miaka 35 jela. Baada ya kufikiria kimbembe cha jela ya kijeshi ya wanaume na kwa vile ameonja kidogo alivyokuwa mahabusu ameomba  abadilishwe  jinsia na kuwa mwanamke na kisha akafungwe jela ya kijeshi ya wanawake, labda kwa kwa kukwepa kalinje kalinje za jela ya wanaume. Manning anajiona kama mwanamke na angependa kuenjoy maisha yake akiwa jela kwa kuwa mwanamke kuliko kuwa mwanaume kama alivyo sasa. Hii ndiyo America akuna kinachoshindikana na lawyer wake ameshikiria kidedea mteja wake atimiziwe kwanza ombi lake ndiyo aanze kutumia kifungo hicho.

No comments: