ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 5, 2013

Mkuu wa Mkoa wa Singida atembelea banda la TMA

 Kaimu Mkurugenzi wa utafiti na matumizi TMA, Dkt Ladislaus Chang’a akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida; Mhe.Dkt  Parseko Kone juu ya jitihada za Mamlaka ya Hali ya Hewa katika kuboresha huduma za hali ya Hewa na katika kuelemisha jamii kuhusiana na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa na umuhimu wa taarifa za hali ya hewa kwa wakulima na jamii kwa ujumla katika maonesho ya Nane Nane mkoani Dodoma
 Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa  Kanda ya Kati  Bw. Waziri O Waziri akitoa maelezo ya kina kwa mwananchi, kuhusu umuhimu wa kutumia na kuzingatia taarifa za hali ya hewa katika mipango na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mhe . Betty Mkwasa (kulia) akipata maelezo kutoka kwa wataalam wa hali ya hewa katika banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa lilipo Nzuguni Dodoma kwenye maonesho ya Nane Nane, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida akisaini kitabu cha wageni.
Wadau mbalimbali katika banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa.

No comments: