ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 6, 2013

Mnigeria akamatwa na kadi za ATM 30 na cheque 8.

Wanigeria wanasifika kwa music,movie,mchezo hadi kutunza mila zao. Lakini upande mwingine pia kuna sifa mbaya sana za mambo ya kihalifu ambayo hufanywa na watu wa hapohapo Nigeria. Kuna habari zilitoka na kuthibitishwa kuhusu kupatikana kwa vichwa vya binadamu kwenye hotel moja huko Nigeria na baadaye polisi kumshikilia mmiliki wa hotel hiyo.

Hivi sasa kijana mmoja ambaye alitambulika kwa jina la Kingsley Mudi, alikamatwa na kadi za ATM 30 za benki tofauti ambazo hadi anakamatwa alikuwa ameshatoa zaidi ya Naila 550, 000 ambazo ni zaidi ya millioni 5 za kitanzania na alikuwa anaendelea kutoa. Unaambiwa pia alikuwa na cheque 8 za UBA Bank zilizokuwa simewekwa sign tayari kwa kutoa pesa. Jamaa kakamatwa na polisi hivi sasa na wizi wa aina hii umeshawahi kutokea hapa Tanzania. Sema ATM kadi 30 jamaa amezidisha sana.

No comments: