Mchakato wa uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) sasa unatarajia kuanza wakati wowote baada ya Msajili wa Vyama na Klabu za Michezo kuipitisha jana kufuatia marekebisho mbalimbali yaliyofanywa katika katiba hiyo kwenye mkutano mkuu uliofanyika Julai 13.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Rais wa TFF, Leodegar Tenga, alisema kuwa kukamilika kwa usajili wa katiba hiyo kunawapa nafasi ya kuruhusu mchakato wa uchaguzi ambao ulisimamishwa kutokana na mapungufu kadhaa yaliyokuwapo awali kutakiwa kuondoshwa na mwishowe marekebisho yaendane na maelekezo kutoka FIFA.
Tenga alisema kuwa baada ya katiba hiyo kufanyiwa marekebisho kwenye mkutano mkuu, waliipeleka kwa msajili ili iidhinishwe kama kanuni na sheria zinavyoelekeza.
"Usajili umepatikana na tunapenda kuishukuru wizara na serikali yetu kwa ushirikiano waliouonyesha. Msajili aliuliza pale alipohitaji ufafanuzi na sisi tulimjibu na sasa tumepata katiba yetu," alisema Tenga.
Alieleza kuwa baada ya mchakato huo kukamilika, sasa kinachofuata ni kuelekea katika uchaguzi ambapo zoezi hilo linatarajiwa kuchukua siku 60 hadi kukamilika.
Aliongeza kwamba mabadiliko hayo ya katiba yalifanyika kwa lengo la kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu ni huru na wa haki.
Aliwataka pia wagombea wenye sifa na wenye sera za kujenga wajitokeze kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
"Tulifanya marekebisho kwa kufuata malekezo ya FIFA. Hakuna aliyepinga, tulipoteza muda mwingi kuboresha... tunashukuru kila kitu kilikwenda vizuri," aliongeza Tenga.
Awali, TFF ilitarajia kufanya uchaguzi wake mkuu Februari mwaka huu lakini haukufanyika kutokana na katiba iliyotarajiwa kutumika katika uchaguzi huo kuonekana kuwa na mapungufu yaliyosababisha wagombea kadhaa kuenguliwa kwa sababu mbalimbali na mwishowe maofisa kutoka FIFA kutua nchini kusikiliza hoja za wagombea waliokuwa wakilalamika baada ya kutemwa.
Tenga ambaye anamaliza kipindi cha pili kuiongoza TFF, alishatangaza kitambo kuwa hatagombea tena cheo cha urais wa shirikisho hilo ambacho anakishikilia tangu Desemba, 2004.
HOJA ZA KUPINGA
Awali, baadhi ya wadau wa soka akiwamo Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla walikaririwa kwa nyakati tofauti wakipinga utaratibu uliotumiwa na TFF kufanya mabadiliko ya katiba hiyo na hivyo kuunga mkono wazo la kutaka msajili asiipitishe katiba hiyo.
Miongoni mwa hoja zilizokuwa zikitolewa ni madai kwamba TFF iliwapa wajumbe ajenda na makabrasha yanayohusu mkutano mkuu siku moja kabla ya mkutano kufanyika wakati ibara 25( 4) ya katiba inaelekeza wajumbe kupatiwa ajenda hizo siku 15 kabla.
Hata hivyo, inaelekea kuwa hoja zote zilizotolewa hazikuonekana kuwa kikwazo kwa msajili ambaye sasa ameipitisha katiba hiyo na kutoa nafasi kwa kina Tenga kuendelea na mchakato wa uchaguzi mkuu wa Shirikisho hilo.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment