NAPE AWAPONDA CHADEMA
- .Adai wanawapotezea watu muda mikutano ya Katiba
- Ajivunia utaratibu uliotumiwa na CCM
- Adai wanachofanya Chadema ni uhuni
- Ampongeza Warioba kukataa maoni ya helkopta
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye
amewaponda Chadema na utaratibu wanaotumia kukusanya maoni ya wananchi
juu ya rasimu ya kwanza ya katiba kuwa ni uhuni na kuwapotezea watu
muda.
Nape akizungumza na waandishi wa habari
mjini Dodoma alipokuwa akielezea ratiba ya vikao vya CCM vya kitaifa
alisema,"sisi tunakutana kupitia maoni ya wanaCCM waliotoa maoni yao juu
ya rasimu ya kwanza ya katiba, lakini wakati sisi tunafanya hivyo
watani zetu wameamua kuwapotezea muda wananchi kwa kufanya uhuni wa
mikutano ya hadhara huku wakijua kuwa ni kinyume na sheria inayoongoza
mijadala ya rasimu hiyo ya katiba"alisisitiza Nape.
Lakini
Nape pia alimpongeza mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya katiba nchini
Jaji Warioba kufuatia kauli yake kuwa atapokea maoni ya taasisi sio ya
helkopta.
"Jaji warioba kawatendea haki hawa watani, sheria
inataka taasisi ikae kama baraza sio ikafanye mikutano ya hadhara.Kasema
sawa sawa, hawatapokea maoni ya helkopta ila ya taasisi sasa sio busara
hawa jamaa kuendelea kupoteza muda wa watu".
"Lakini najua
wataendelea tu kwasababu inabidi watoe hesabu ya pesa walizopewa kwa
kazi hii.Watafanyaje sasa zaidi ya kuruka na chopa ili wakidhi matakwa
ya waliowatuma,ndo tabu ya vibaraka!"alisisitiza Nape.
Kuhusu
vikao alisema sekretariete ya CCM imekutana kwa siku tatu mjini Dodoma
kuandaa kamati kuu inayokutana kesho na Halmashauri kuu inayokutana
tarehe 24 -25/08/2013.
4 comments:
Nape huo wivu badala ya kuongea mambo yatakayo msaidia mtanzania umekalia chadema hebu angalia Mbeya chadema walivyo jaza!
Wanaopoteza muda ni ccm mafisadi wamejazana kwenye chama maendeleo hayaonekani wananchi wamechokaa viongozi wanajali familia zao ukweli tumechoshwa na udhalimu ccm.
Watu nyomiiiiii
Tushachoka na ccm wao ndio wanaopoteza muda wanajali matumbo yao wanasahau wenzao.
Post a Comment