ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 22, 2013

MAALIM GURUMO ATANGAZA RASMI KUSTAAFU KUIMBA ,MUZIKI

Wadau wakipiga picha na Maalim Gurumo


KAMANDA na gwiji wa muziki wa dansi katika bendi ya Msondo Maalim Muhidin Gurumo (73) ametangaza kuacha rasmi kujighulisha muziki wa dansi kama jinsi aliyoifanya kwa muda wa miaka 53.

Gurumo aliyasema hayo leo saa sita mchana katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO Dar es Salaam.

“ Leo nimekuja kuwaga rasmi wanamuziki na wapenda muziki na waliokuwa mashabiki wangu kwa ujumla , sitaki tena muziki ila ikumbukwe kwamba muziki ni asili yangu ila sasa nimeamua kustaafu kwa moyo mmoja hivyo naahidi kuwa nitawasaidia wanamuziki wanaobaki kwa uhuru na moyo mmoja” alisema Gurumo. ), jijini

Wakati huohuo, Gurumo anasema anastaafu akiwa hana kitu cha maana katika tasnia ya muziki wa dansi licha ya kuutumikia na kufanya kazi kwa moyo wake wote kwa kipindi cha miaka 53 iliyopita.

“Nilianza kuimba nikiwa kijana wa umri wa miaka 20 mwaka 1960 na tangu hapo sikuwahi kubadili kazi lakini sasa nastaafu ilhali nikiwa sina hata baiskeli” alisema Gurumo.

Wakati huohuo Mratibu mkongwe nchini wa matamasha mbalimbali na muanzilishi wav iota na kumbi nyingi za burudani hapa jijini Dra es Salaam Juma Mbizo anatajwa na Gurumo kuwa ndiye atakuwa mratibu katika tamasha maalum litakaloandaliwa la kumuaga .
Katika kamati hiyo pia wamo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya The African Stars Entertainment ‘Aset’ Asha Baraka, Mdau wa burudani Said Mdoe, Richardson Sakalla, Mkurugenzi wa bendi ya The Kilimanjaro ‘Wana Njenje’ Waziri Ally.

“Hii kamati imeundwa ili ili iweze kumsaidia katika kumuandalia tamasha maalum , hivyo ipo siku tutaweka wazi tumeandaa kumfanyia nini mkongwe huyu wa dansi kadhalika siku hiyo ya tamasha lake ndipo atakapoimba kwa mara ya mwisho na kuanzia leo hatopanda katika jukwaa lolote kuimba” alisema 

Mbizo aliongeza kwa kusema kuwa Gurumo amepata ridhaa kutoka kwa wanamuziki wenzake wote kabla kufikia uamuzi huo wa kustaafu muziki na kwakuwa ameimba kwa miaka mingi sasa mi wakati wake wa kupumzika.

Wosia wake kwa wanamuziki wanao baki anasema yeye anawaasa wapige muziki wa nyumbani hasa waliokuwa wakipiga bendi ya Msondo “Wapige muziki ambao tulikuwa tunapiga sisi zamani tofauti na hivi sasa ambapo wanamuziki na vijana wengi wanakimbilia katika muzikiwa Bongo Fleva ambao ni muziki unaokwenda na wakati lakini ni wa kupita.
Mwisho anamalizia kwa kusema kwamba kustaafu kwake hakuzuii yeye kutoa ushauri au kufundisha wanamuziki na wapiga ala kwani anakipaji cha kumfundisha mpigaji wa chombo chochote kwa kutumia mdomo wake.

Kadhalika Gurumo anasema kwamba katika nyimbo alizowahi kuimba wimbo anaoupenda ni wimbo wa ‘Usimchezee Chatu’ ambao aliumba kipande kidogo mbele ya Waandishi wa Habari na katika wanamuziki wa Bogo Fleva anampenda Naseeb Abdul ‘Diamond’. 


Gwiji Maalim Gurumo aliyekaa katikati, kushoto ni Meneja wa Bendi ya Msondo Kibiriti na Mratibu wa tamasha Juma Mbizo.Waliosimama ni waandishi wa habari Khadija na Hemed Kivuyo (ITV).Hapa ni mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo.

No comments: