Dar es Salaam. Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inatarajia kuanzisha umoja wa fedha katika nchi wanachama wa jumuiya ili kupata sarafu moja itakayotumika kwa nchi hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, msemaji wa Wizara hiyo Verdastina Justinion alisema mbali na kuanzisha sarafu moja ya Jumuiya, nchi wanachama wamekubaliana kuongeza kiwango na kasi ya mtangamano wa masoko ya fedha na mitaji.
Wamekubaliana pia kuhuisha sera za kibajeti za nchi wanachama na kuunda Benki Kuu moja ya Jumuiya (EACB) itakayosiamamia sera moja ya fedha.
“Lengo la kuanzishwa kwa umoja huo wa fedha ni kujenga ukanda tulivu wa kifedha utakaoharakisha kusaidia ukuaju wa biashsra na shughuli za kiuchumi ndani ya Jumuiya na kwamba mpango wa kuwa na sarafu moja ya Jumuiya unatarajia kukamilika mwaka 2024,” alisema Justinion.
Justinion alisema vigezo vya nchi hizo wanachama kushiriki katika kuandaa sarafu moja ya Jumuiya hiyo kiwango cha juu cha mfumuko wa bei kisichozidi asilimia 8, kiwango cha juu cha nakisi ya bajeti ikijumuisha misaada kisichozidi asilimia 3 ya pato la taifa, kiwango cha juu cha deni la taifa kisichozidi asilimia 50 ya pato la taifa na akiba ya fedha za kigeni ya kutosheleza mahitaji ya miezi minne na nusu.
“Hatua hii ya kuanzisha sarafu moja ya Jumuiya inatokana na kufanyika kwa mchakato wa uundaji wa Umoja wa Fedha wa Afrika Mashariki ambao ulianzishwa na kikao cha 15 cha baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki kilichofanyika Machi 2008 na kuidhinishwa na kikao cha wakuu wan chi wa Jamuiya hiyo,” alisema Justinion.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment