ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 22, 2013

NDEGE NDOGO YA TANZAIR KUNUSURU ABIRIA WAKE BAADA YA KUTIA HITIRAFU IKIWA ANGANI NA KUTUA LAKE MANYARA

Habari zilizoufikia mtandao huu hivi punde kutoka Mkoani Arusha zinaeleza kuwa Ndege Ndogo ya Shirika la Ndege la TANZAIR iliyokuwa ikitokea Mjini Bukoba kuelekea Jijini Dar es Salaam, imelazimika kutua katikati ya Ziwa Manyara lililopo Mkoani Arusha ili kunusuru abiria wake sita (6) waliokuwamo katika ndege hiyo baada ya kupatwa na hitilafu kwa kuzima ghafla kwa Injini moja wakati ikiwa hewani.


Aidha imeelezwa kuwa katika tukio hilo ni abiria watatu tu ambao wamepatwa na majeraha makubwa huku wakipelekwa kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Sirialni ya Mkoani Arusha, huku wengine wakitazamiwa na kuchunguzwa kabla ya kuruhusiwa kuweza kuendelea na safari.


Rubani wa ndege hiyo alilazimika kutaka kutua ghafla katika Uwanja wa Arusha, kutokana na Hitilafu hiyo, lakini alishindwa baada ya kuona mtikisiko ukizidi na kuamua kuielekeza ndege hiyo katikati ya Ziwa hilo, ambapo alifanikiwa kutua salama na baadhi ya Boti na mitumbwi iliyokuwa karibu iliweza kusogea na kutoa msaada wa kubeba abiria hao na kuwasogeza nchi kavu na baadaye ilifika Helkopta ambayo iliweza kutoa msaada zaidi.

No comments: