ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 18, 2013

JK ATEMBELEA CAPITOL HILL

 Rais Dkt Jakaya Kikwete akiongozana na Mhe. BernardWaziri Membe na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula tayari kuelekea Capitol Hill  kuendelea na ziara yake nchini Marekani. Rais Kikwete aliwasili Washington, DC  leo Jumatano Sept 18, 2013 asubuhi  akitokea California
Rais Dkt Jakaya Kikwete akiongea na Halima Mamuya na H.V. Street wamiliki wa AmeriTan International ya Louisiana

Juu na chini ni Rais Dkt Jakaya Kikwete akijiandaa kuingia kwenye gari kuelekea Capitol Hill kuendelea na ziara yake nchini Marekani
Gari lililomchukua Rais Dkt. Jakaya Kikwete likiondoka kuelekea Capitol Hill.

6 comments:

Anonymous said...

Capitol Hill anakutana na nani---muhimu kufafanua,plus lengo la ziara yake ni nini?

Anonymous said...

Lengo ya ziara yake ni kutembea kama ilivyoaanishwa mwanzo wa hii posting!
Kutembea ni kusoma mengi!

Anonymous said...

Hivi hii ni mara ya ngapi kufika huko US maana sijawahi kumuona Jacob Zuma,Yoweri Museveni,James Banda Rupia au rais mwingine anayetembea sana kama huyu huku KODI zetu zikiteketea kwa sana bila kueleweka... Naomba nieleweshwe wadau wabeba boksi wote duniani

unanimous said...

Kuna nini anajifunza au anafundishwa?

Anonymous said...

Usiwe na wivu mdau, yaelekea wewe ni kipofu wa Chadema au CUF? Huyu ni Rais wetu na amekuja kikazi na huna haja ya kujua details za ziara yake! Umesikia kitu kinachoitwa "DIPLOMACY"? check webster dictionary itakusaidia if you are sober! Karibu Rais JK, wengi tupo excited kwa ujio wako.

jitinde said...

mbona alipotembelea mwanza hamkuhoji anatembelea nini? hao wanaohoji kafuata
nini hata kodi hawalipi wamejazwa chuki na wanasiasa wapiga makelele kwa jazba! hivi unakiwa na akili timamu unashindwa kiujua rais anapata manufaa gani akifanya ziara nchi za nje? na ameambatana na nani. kwa nini? acheni siasa za kishamba