Kadhalika, Dk. Mengi ameahidi kuwapa zawadi wanafunzi 78 wanaoatarajia kumaliza kidato cha nne mwaka huu ikiwa watafaulu kwa daraja la kwanza kila mmoja.
Dk. Mengi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 11 na maadhimisho ya miaka 13 ya shule hiyo, aliwaambia wazazi, wanafunzi, walimu na wageni waalikwa kuwa kila mtu mwenye uwezo wa kifedha ana wajibu wa kusaidia wale wasiokuwa na uwezo hususani katika sekta ya elimu.
Kuhusu moyo wa kusaidia watu wengine, alisema hata mtu awe na mamilioni ya fedha akifa hawezi kuzikwa nayo na kwamba njia nzuri ya kuzitumia ni kuwasaidia wasiokuwa na uwezo ili waweze kupata elimu ambayo itawasaidia maishani mwao.
Dk. Mengi alisema elimu ni njia pekee ya kumsaidia mtoto na kuwataka wanafunzi wanaotarajia kumaliza kidato cha nne mwishoni mwa mwaka huu kuacha kuwa na ndoto ndogo badala yake wawe na ndoto kubwa.
“Maisha yenu nyinyi wanafunzi yapo mikononi mwenu kwa hiyo lazima mkazanie elimu mnayopewa ili iweze kuwasaidia maishani mwenu,” alisema na kuwataka siku zote kusema maneno ya Kiingereza kuwa “I can, I will and I must” yakimaanisha kuwa nitaweza, nitafanya na lazima nitaweza.
Kwa upande wa zawadi alizowaahidi wanafunzi watakaopata daraja la kwanza, Dk. Mengi aliwataka kutumia fursa vizuri na kuahidi kuupatia uongozi wa shule hiyo Sh. milioni mbili ili zisaidie kuwafungulia akaunti wanafunzi wote ili zawadi hizo zitakapotolewa ziingizwe benki moja kwa moja.
Muasisi wa shule hiyo, Profesa Anna Tibaijuka alisema kitendo kilichofanywa na Dk. Mengi sio cha kawaida na kinafaa kuigwa kwa kuwa ametoa mchango mkubwa ambao utaisaidia jamii moja kwa moja.
CHANZO: NIPASHE
1 comment:
DR. Mengi hayo ndio maneno ya watu wenye akili wanayozungumza wanapoka uwa kwenye dhifa za kijamii. Mungu aendelee kukuwezesha kwa kila namna ili wale wanaohitaji msaada waweze kufikia pale wanapotamani. Sio wale wanaoenda kwenye mikutano na mashati ya kijani, kubeba watoto na wanashindwa hata kuwapa hata sh. 1000. ya kununua kiatu cha mguuni!! Siasa za uchwro hazifai kwa kweli. Tutizame jamii inakoelekea na tunahitaji elimu sana sio blablaaa.
Asante.
Post a Comment