ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 21, 2013

CHRIS BROWN ARUDISHWA TENA REHAB KWA MIEZI 3 BAADA YA KUHARIBU GARI YA MAMA YAKE.

By Nixl Carter 
Jaji James Bradlin ametoa amri ya kumrudisha rehab Chris Brown kwa muda wa siku 90 ili aendelee na matibabu ya kudhibiti hasira ikiwa ni siku chache baada ya kutoka huko na kuendelea kuhudhuria matibabu kama mgonjwa wa nje.

Amri hiyo imetolewa mahakamani Jumatano (November 20) kufuatia ripoti iliyotolewa na afisa aliyekuwa anaangalia muenendo wa kipindi cha probation alichopewa Chris Brown tangu ampige vibaya Rihanna mwaka 2009.
Ripoti hiyo ilionesha kuwa Chris alijikuta katika mood ya hasira nyingi na kuvunja kioo cha gari la mama yake akiwa katika eneo la rehab mwanzoni mwa mwezi huu. Lakini pia imeonekana kuwa kuna mengi yalitokea wakati wa tukio la Breezy kumshambulia mtu October 26 huko Washington DC.

Jaji James Bradlin pia alitoa amri inayomtaka ‘Don’t Work Me Up’ hit maker huyo kufanya kazi za kijamii kwa masaa yasiyopungua 25 kwa wiki.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 25, akiwa na mwanasheria wake walikubali uamuzi huo bila pingamizi lolote.

Hii inamaanisha kuwa albam yake ya ‘X’ iliyokuwa inatarajiwa kutoka mwaka huu inaweza kuchelewa zaidi kuliko ilivyotegemewa mwanzoni kutokana na muda atakaoutumia rehab.

No comments: