ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 1, 2013

HUU NDIIO UTAJIRI WA WEMA SEPETU LICHA YA KUSUSIWA NA BONGO MOVIE KWENYE MSIBA WA BABA YAKE LAKINI VIONGOZI WA JUU WA SERIKALI WAFURIKA


Well, well, well! Hiki ni kitu ambacho kila mmoja anapenda kukifahamu. Wema Sepetu ni tajiri kiasi gani? Ni ngumu kusema exactly mrembo huyu ana shilingi ngapi benki, lakini mambo anayofanya yanatupa jibu la wazi kuwa, Wema ana mkwanja mrefu. So hebu tuangalie mangapi makubwa yaliyohusisha fedha nyingi aliyoyafanya kuanzia mwezi June, 2012.
1. Thamani ya nyumba yake
Wema Sepetu aliwaacha hoi watu wengi baada ya kuonesha nyumba yake mpya exclusively kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV. Alisema thamani ya nyumba yake hiyo ilifikia shilingi milioni 400 na hiyo ni tofauti na karibu shilingi milioni 30 za kuipamba ndani. Hiyo ilikuwa ni tarahe za mwanzo za mwezi June, 2012. Kwa picha zaidi nenda soma zaidi
Sebule
Wema Sepetu akielezea jambo
Wema na Zamaradi Mketema wa Clouds TV
 
 Sehemu ya nje ya nyumba
Dj Choka alikuwa miongoni mwa watu waliotembelea nyumba hiyo
2. Uzinduzi wa filamu yake Superstar 
Katika historia ya Bongo Movies, hakuna filamu iliyowahi kuwa na uzinduzi wa nguvu kama wa filamu ya Wema ambayo hata hivyo haijawahi kutoka, Supastar. Katika uzinduzi huyo, Wema alimdondosha muigizaji namba moja wa kike nchini Nigeria, Omotola Jalade ambaye alimpeleka kwenye event iliyofanyika Giraffe Hotel Ocean View ambako watu mbalimbali walikutana kubadilishana mawazo na Omotola. Hiyo ilikuwa ni baada ya kushindwa kufika kwa wakati.
Awali ulifanyika uzinduzi wa filamu hiyo yenye mastaa kibao akiwemo yeye mwenyewe, TID, Shetta, Mwinyi Machozi, Chaz Baba, Barnaba na wengine kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro ambako mastaa wote wa orodha A nchini walihudhuria huku Shaa na Shilole wakiwa miongoni mwa wasanii waliotumbuiza.
Ben Kinyaiya na Irene Uwoya
Ray, Dr Cheni, Steve Nyerere nao walihudhuria

Shughuli nzima hiyo iliyofanyika mwishoni mwa mwezi June mwaka jana, ilitumia takriban shilingi milioni 40 zikiwemo gharama za kumlipa Omotola.

3. Gari anayomiliki Kwa sasa Wema anamiliki gari aina ya AUDI Q7 ambayo thamani yake inafikia shilingi milioni 80. Awali ya hapo alikuwa na Toyota Mark X ambayo thamani yake ni takriban shilingi milioni 60.
Wema akiwa na mkoko wake4. Thamani ya ofisi na kampuni yake, Endless Fame Films February 21, Wema alifanya uzinduzi maalum wa ofisi za kampuni yake ya Endless Fame Films zilizopo Mwananyamala jijini Dar es Salaam ambazo thamani yake ni takriban shilingi milioni 70.
5. Gharama anayotumia kuwatunza mbwa wake, Vanny na GucciMtandao wa Global Publisher jana uliandika, “KWA wale wenye hali ngumu kimaisha wataishia kusema; ni kufuru iliyoje kwani staa wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu hivi karibuni amewafanyia mbwa wake wawili ‘shopping’ iliyogharimu dola 4,000 za Kimarekani (zaidi ya Sh. milioni 6.5 za madafu). 
Wema aliteketeza kiasi hicho cha fedha kwa kuwanunulia mbwa hao pafyumu, viatu na nguo, alivyoagiza kutoka nchini China, lengo likiwa ni kuhakikisha wanaishi katika mazingira mazuri. 
Akizungumzia ‘shopping’ hiyo nyumbani kwake Kijitonyama, jijini Dar, Wema alisema: “Kiukweli nawapenda sana hawa mbwa, ukinipasua roho yangu utawakuta ndiyo maana nataka wavae na kunukia vizuri, kinyume chake siwezi kuwa na amani.
Vanny na Gucci wakicheza
Vanny
Vanny
Gucci akiwa amelala
“Najua watu wanaweza kushangazwa na kitendo cha mimi kutumia kiasi hicho cha fedha lakini sioni kama ni tatizo kwani ni kitu ambacho kinanipa furaha katika maisha yangu.” 
Leo kupitia Instagram, Wema ameandika, “Vanny ake heading to da hospital…. my poor baby is sick…. nat happy at all, hope u get better soon.”

6. Shilingi milioni 13 alizomtolea Kajala baada ya kusomwa hukumu yake 
Wema Sepetu alimake headline baada ya kutoa mfukoni mwake shilingi milioni 13 kulipa faini aliyopigwa muigizaji mwenzie Kajala Masanja aliyehukumiwa kwenda jela miaka mitano ama kulipa kiasi hicho cha fedha. 
Akizungumza exclusively na Bongo5, Wema amesema hakufikiria mara mbili kutoa kiasi hicho cha fedha. “Kusema kweli wanasemaga kwamba kutoa ni moyo so naamini what I did is best, nimetoa kwasababu I had to do it and sikuthink twice kuhusu kufanya hivyo,” amesema Wema. 

“Nimefanya kama namsaidia rafiki yangu kama namsaidia ndugu yangu na sidhani kama ingekuwa ni kitu kizuri kumuona mwenzako anaingia kwenye dhahama, kwenye tabu, kwenye mateso na wakati nina uwezo wa kumsaidia kwahiyo I just did what I had to do.” 

7. Jinsi anavyomwaga hela kwenye sherehe mbalimbali 


Katika katika sherehe za 8020 Fashion’s Woman Celebration zilizofanyika kwenye siku ya wanawake duniani, Wema aliuteka ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya kumwaga mihela kwa mwimbaji maarufu wa Taarabu nchini, Khadija Omar Kopa. Wema alimwaga mkwanja huo kumpongeza Khadija kwa kukonga moyo wake. 
Hayo ni machache tu tunayofahamu na kwa hesabu hizo bila shaka utakubaliana nasi kuwa Wema Sepetu ana mkwanja mrefu!!!

4 comments:

Anonymous said...

WALOACHA KWENDA HAWAKUA NA BUSARA KUSEMA KWANINI HAWAKWENDA .WATU WAZIMA HOVYO WANGESEMA WALIKUA BUSY KULIKO KUSEMA KWANI YY ANAKUJAGA KTK MISIBA YETU .KUMBUKEN ALIPOKUFA KANUMBA WALIKWENDA HATA WASIOMJUA.
KUMBUKENI WAHENGA WALISEMA KILA MTU MA KICHWA CHAKE .KUZIKWA KWA MTU NI VILE ALIVYOJAALIWA
KWANI MLIVYOACHA KIMETOKEA NINI???
UMASIKINI WA ROHO MNASHINDANA MNA MUNGU NDO MGAWAJI .SAFIRIENI NYOTA ZENU SIO ZA WENZENU

Anonymous said...

Tena hao ambao wandai Wema hakwenda walipopatwa na misiba twawaona humu kwenye uzinduzi wa filamu yake, si wangemsusia pia? Hawana mana kabisa!

Anonymous said...

Hao wote washenzi kwanza wachovu!wema anarock ,mzuri,mrefu..she is a star ndo mana wanamuonea wivu..wasanii wabongo movie wote choka mbaya..Wema your good girl dont worry about people..wanatamni wakushushe ila ndo hawawezi.

Anonymous said...

Hao wote washenzi kwanza wachovu!wema anarock ,mzuri,mrefu..she is a star ndo mana wanamuonea wivu..wasanii wabongo movie wote choka mbaya..Wema your good girl dont worry about people..wanatamni wakushushe ila ndo hawawezi.