ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 1, 2013

MTU MMOJA YUPO ANASHIKILIWA NA POLISI BAADA YA KUFYATUA RISASI KWENYE UWANJA WA NDEGE LOS ANGELES


Mtu mmoja anashikiliwa na polisi baada ya kufyatua risasi na kujeruhi na kujehuhi wakaguzi wa TSA wanaoogakua abiria kabla ya kuingia kwenye ndege. Mtu huyo ambaye hajatajwa jina bado ameleta kizazaa hicho mida ya saa 3:20 asubuhi saa za California na kuleta taharuki kwa abiria waliokuwa uwanjani hapo kwenye safari zao nje na ndani ya Marekani. kutokana na watu waliokuwepo uwanjani hapo wamesema walisikia milio ya risani ipatayo 8 mpaka 10 na kusababisha vurugu ya watu waliokuwepo kwenye tukio kukimbia ovyo kujaribu kusalimisha maisha yao wengine walijaribu kuzima simu zao wasije wakajulikana walipo na mtu huyo ambaye baadae alidhibitiwa kwa kupigwa  risasi ambayo haikumuua.

Kwa sasa hivi FBI wanafanya uchunguzi wa kumjua mtu huyu na sababu gani zilizomfanya afyatue risasi na habari zilizotufikia sasa hivi yule mfanyakazi wa TSA aliyepigwa risasi amefariki wakati alipokua anakimbizwa hospitali

1 comment:

Anonymous said...

Kabu na Tillo + Sepetu family, be strong homies, Pamoja