ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 22, 2013

HUYU NDIYE RAGE ALIWAI KUTUHUMIWA KWA UPOTEVU WA PESA KATIKA NGAZI KUU ZA MPIRA WA MIGUU TANZANIA NA KUTUPWA JELA LAKINI SASA NDIYO KIONGOZI WA TIMU KUBWA TANZANIA


Mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage amewasili Dar es salaam Tanzania leo akitokea Sudan ambapo alipokelewa na baadhi ya Wanachama wa Simba kwenye Uwanja wa ndege wa mwalimu JK.Nyerere.
Waandishi wengi walikua na maswali mengi kuhusu yeye kusimamishwa kuwa Mwenyekiti wa Simba lakini akayapangua kwa kusema kesho mchana ndio atazungumza na Waandishi kuhusu kila kitu ila sentensi moja iliyonyakwa na millardayo.com ni ‘taarifa za kusimamishwa Uwenyekiti sijazipata, ninachojua mimi bado ni Mwenyekiti wa Club ya Simba’
. Rage amewahi kutumikia kifungo jela kwa upotevu wa mamilion leo ndiyo kiongozi wa timu kubwa Tanzania. Rage ndiyo jembe mwenye sauti katika timu hiyo kubwa walitangaza kumng'o lakini wameishia kumpokea kwa shangwe na vifijo akitokea Sudan. 
Baadhi ya Wanachama wa Simba wakicheza wakati wa mapokezi.

1 comment:

Anonymous said...

si ndo siasa ya ccm hiyo na ya kitanganyika mafisadi wanapoa kama miaka halafu baadaye wanarudi tena kwenye jamii na kuhuriri utumbo utumbo chunguzeni mtaona