November 5 2013 ndio stori zilianza kusambaa baada ya ripoti ya Mbunge wa viti maalum Easter Bulaya bungeni iliyohusu biashara ya dawa za kulevya huku ikitaja idadi ya Watanzania waliofungwa nchi za nje kwa kujihusisha na biashara hiyo pamoja na baadhi ya wanaohusika ndani ya nchi.
Baada ya ripoti hiyo, Easter anakiri usiku huo alipata msg nyingi za watu kuhofia maisha yake na nyingine zikimpa pongezi kwa ujasiri alioufanya, ujasiri ambao pia Marehemu Amina Chifupa aliwahi kuufanya.
Kwenye taarifa mpya aliyoitoa kwa millardayo.com Easter Bulaya amekiri kupokea vitisho vya maisha kutoka kwa watu asiowafahamu kitu kilichofanya aanze kubadili hata jinsi ya kuishi.
‘Namshukuru Mungu kwamba niko hai na nimefurahi kupigiwa simu na Wachungaji na Sheikh wakiniombea baada ya kuiona ripoti yangu ila simu za kutishiwa maisha nimepigiwa mara mbili na private number… mwanzo ilikua msg za pongezi tu na kuhofia maisha yangu kwa ujasiri nilioufanya ila sasa ni vitisho mpaka nyumbani kwangu’ – Easter
Kwenye sentensi hii, Easter anasema ‘tulimaliza bunge Jumamosi vitisho vya simu vikaanza Jumanne vikidai vitanikomesha, naamini mtu kama siku zimefika huwezi kukimbia kivuli chako kama wameamua kukufanyia la kukufanyia watakufanyia tu… kuna siku mtu alikuja nyumbani kwangu akagonga saa tano usiku nikamuuliza wewe nani ili nikufungulie akakataa kutaja jina lake na kusema wewe njoo nifungulie nina shida na wewe, nikamwambia sikufungulii ndio akaniambia we kataa lakini tutakupata tu’
Kwa kumalizia, Mheshimiwa Easter Bulaya anasema ‘mimi sitishiki na nitaendelea kufanya hii kazi kwa moyo wangu wote kwa sababu vijana wamenichagua’
No comments:
Post a Comment