ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 27, 2013

411,127 KATI YA 427,609 KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA TANZANIA 2014

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu –TAMISEMI, Jumanne Sagini (picahni) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya wanafunzi 411,127 kati ya 427,609 sawa na asilimia 96.15 waliofaulu mtihani wa darasa la saba 2013 wataanza kidato cha kwanza mwaka ujao.

Kati yao wasichana ni 201,021 na wavulana 210,106 na huku kiwango cha wanafunzi waliochaguliwa mwaka huu wakiwa wameongezeka kwa asilimia 31.37 ikilinganishwa na asilimia 64.78 waliochaguliwa awamu ya kwanza mwaka huu.

Matokeo yanaonesha kuwa jumla ya wanafunzi 427,609 (wavulana 218,093 na wasichana 209.516) walifaulu kwa kupata alama A-C kati ya 844,938 waliofanya mtihani ikiwa ni sawa na asilimia 50.61 … takwimu zinaonesha ongezeko la asilimia 19 la ufaulu ikilinganishwa na asilimia 30.6 mwaka jana.CREDIT:FATHER KIDEVU

No comments: