ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, December 22, 2013

ASIYEKUBALI KUFUNGWA SI MSHINDANI ASEMA MANJI

Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji akiongea na wamahabari

Mwenyekiti wa timu ya Yanga amesema amekubali kipigo cha goli 3-1 kutoka kwa wapinzani wa jadi mnyama Simba katika mchezo wa nani mtani Jembe uliochezwa uwanja wa Taifa jana Jumamosi Dec 21, 2013. Yusuf Manji akiongea katika mkutano na  waandishi wa habari mapema leo alisema kipigo hicho hakuna wa kulaumiwa ni sehemu ya mchezo si kosa la kocha, wachezaji labda wakuaumiwa niwe mie, tumefungwa kutokana na kujiamini kupita kiasi.

Katika mechi ya Jana imepokewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa Yanga Ughaibuni wengi wao walitupia lawama kwa uongozi kwa kuendelea kusajili wachezaji toka Simba na kitu kingine kuwapa nafasi wachezaji wapya kucheza mtanange wa jana kwa madai ya kutokua na maelewano na wachezaji wa zamani mashabiki hao waliendelea kusema hawakuona sababu ya kumchezesha Juma Kaseja na Emmanuel Okwi tunawachezaji wengi wazuri na ambao wamecheza muda mrefu pamoja kulikua hakuna sababu ya kuwachezesha wachezaji hao.

Kwa upande wa mashabiki wa Simba Ughaibuni palikua hapatoshi kwenye Mafacebook, what's up, text msgs ili mradi ni kero kwa kwenda mbele, ushindi wa Simba wa 3-1 dhidi ya Yanga haukutegemewa na mashabiki wengi Ughaibuni kutokana na ukweli kwamba usajili wa Yanga umekamilika lakini baada ya kipigo hicho Mashabiki wa Simba waliwadhihaki mashabiki wa Yanga kutwa nzima ya jana.

No comments: