CEO wa Vizion One Home Health Services Abdallah Kitwara pamoja na mkewe wakiwasili kwenye ukumbi huku wakilakiwa na John Sitta mmoja ya wakurugenzi wa kampuni hiyo siku ya Ijumaa Dec 20, 2013 siku kampuni hiyo ilipofanya mnuso wa nguvu wa waliouita Happy Holidays pamoja na kusherehekea mnuso huo Bwn Abdallah aliwapa wafanyakazi wake bahasha za asante kwa ufanisi na kujituma kwao katika kuitumikia kampuni hiyo ambayo inakuwa kwa kasi mwaka hadi mwaka.
Meza kuu kutoka kushoto ni CEO wa Vizion Bwn. Abdallah Kitwara, Mkewe na mmoja ya wakurugenzi wa kampuni hiyo Bwn. John Sitta.
CEO wa Vizion One akisalimiana na wageni waliofika kwenye sherehe hiyo wakiwemo wafanyakazi wake muda mfupi alioingia kwenye ukumbi wa Oxfford uliopo Lanham, Maryland.
CEO wa Vizion One Bwn. Abdallah Kitwara pamoja na mkewe wakisalimia wageni na wafanyakazi wake zikiwemo kampuni zinazofanyakazi chini ya kampuni hiyo na baadae kuwashukuru kwa uajibikaji na kujituma kwao ukiwemo ufanisi uliotukuka uliopelekea kampuni ya Vizion One kufika hapo ilipofika leo upendo, ushirikiano na kufanyakazi pamoja kama wanafamilia ndio nguzo ya mafanikio ya Vizion One. Pia aliwatambua uwepo wao marafiki zake waliocheza nae mpira enzi hizo.
Magrett mmoja ya wakurugenzi wa Vizion One akiongea machache na kuwatambulisha wafanyakazi waliopo kwenye kitengo chake.
Fatuma Kitwara dada mdogo wa CEO wa VIZION One akiongea machache.
mmoja ya wafanyakazi wa Vizion One akitoa yake ya moyoni ya jinsi gani anafurahia kuwa mfanyakazi wa Vizion One .
Mmoja ya wafanyakzi wa Vizion One akiongea machche na kushukuru na kufarijika kufanyakazi Vizion One.
Wakurugenzi wa Vizion One kwa niaba ya CEO wakimkabidhi mmoja ya mfanyakazi (kati) bahasha ya asante, bahasha hizo zilitolewa pia kwa wafanyakazi wengine.
Mmoja ya wafanyakazi wa Vizion One (kati) akipozi kwa picha baada ya kupokea bahasha yake ya asante.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Mwendeshaji wa Vijimambo Dj Luke akisalimiana na CEO wa VIzion One Mr. Abdallah Kitwara.
4 comments:
Inapendeza sana kuona watanzania wanafanya mambo mazuri hasa katika kuwekeza kiuchumi na kuwa kuwa kampuni kubwa kwenye nchi kubwa kama Marekani. Hongereni sana Vizion One!
This is great! Watanzania wooote tuwe na kiu ya maendeleo, sio wale mnao enda nchi za Watu kupiga umbea, kusengenya na kununua Gucci,Prada na all the fake things in life! Be inspired! Be motivated! Work hard! Help others to get somewhere and not just blah blah! Watanzania tubadilike- sio ku ng'ang'ania nchi za Watu halafu hakuna chochote cha maana unachokifanya! ! Good job Vizion One.
Na pia kuona mtanzania anatoa ajira kwa watanzania na kubadilisha hali ya uchumi majumbani mwao. Mungu akubariki kaka Abdallah kwani amesaidia jamii yetu sana tuu.
Yaani ni furaha kubwa huyu kaka anavyofanya.I wish angeweza kufungua na huku new york.
Post a Comment