Naibu wa Waziri wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia January Makamba.
Kauli hiyo ya Makamba ameitoa leo wakati wa kufungua kongamano kubwa la siku moja la Umoja wa Madereva wa pikipiki Mwanza lililofanyika katika uwanja wa michezo wa Nyamagana Jijini hapa, alisema kwamba kuna baadhi ya watu wameanza kuhoji ujio wangu Mwanza “Niko hapa kwa ajili ya shughuli hii mliyonialika bali kuja kushiriki Kampeni muhimu ya Bima ya Afya kwa ajili ya Usalama wa badae” na si vinginevyo.
Kabla ya kongamano hilo madereva hao wa bodaboda walifanya maandamano toka makao makuu ya ofisi zao yaliyopo mtaa wa malango mmoja wilayani Nyamagana jijini Mwanza hadi katika uwanja wa historia wa Nyamagana.
Wadau wa Bodaboda wakiingia uwanja wa Nyamagana.
Ndani ya uwanja wa Nyamagana madereva wa Bodaboda wamejitokeza kiasi cha kutosha.Wakizidi kumiminika viwanjani hapo kuhudhuria kongamano lao.Naibu wa Sayansi na Teknolijia ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli mhe. January Makamba akiingia katika uwanja wa Nyamagana kushiriki kongamano la Bima ya Afya kwa waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda wa mkoa wa Mwanza.
No comments:
Post a Comment