ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, December 29, 2013

Misa ya Kiswahili - Nia Binafsi, Shukurani na Kuombeana, leo Jumapili 29 Decemba 2013

 Mapadri kutoka kushoto Fr. Shao, Fr. Leandrah Kimario na Fr. Jean Tambwe wakiongoza misa takatifu ya kiswahili iliyofanyika Baltimore, Maryland ya kuadhimisha miaka 3 ya misa ya Kiswahili DMV  hivi karibuni.

Wapendwa Wote, 

Twawatakia heri na fanaka za sikukuu ya Noeli na Mwaka Ujao

Mnakaribishwa sana kwenye ibada ya misa takatifu ya lugha ya kiswahili kwa nia binafsi, shukurani na kuombeana.

Ibada itafanyika katika kanisa takatifu katoliki la Mtakatifu Edward (St Edward Parish)
901 Poplar Grove St, Baltimore, MD 21216, Phone: (410) 362-2000
Tarehe 29 Decemba 2013. Saa nane kamili mchana (2:00 PM).
Baada ya ibada tutakutana kwa mlo na viburudisho.
Karibuni sana na unaombwa uwataarifu na kuwakaribisha ndugu, marafiki na jamaa zako.
Kama una swali au maoni unakaribishwa kujibu barua pepe hii.
Asante sana kwa niaba ya Baba Paroko, Evod Shao

No comments: