ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, December 21, 2013

NDUGU WA MTANZANIA ALIYEFIA AFRIKA KUSINI WANATAFUTWA


 Watanzania waishio Johannesburg wanawatafuta ndugu, rafiki au jamaa wa Shiraz Abeid Juma (pichani), ambaye sasa ni marehemu. Shiraz alifariki wiki hii na kuzikwa siku ya Jumanne huko Johannesburg, Afrika Kusini.

Marehemu alifika Afrika Kusini akitokea eneo la Mpendae kule Zanzibar kama nyaraka alizoacha zinavyoonyesha. Namba za simu zilizokuwa kwenye vitabu vya marehemu hazipatikani. Kwa yoyote mwenye kumfahamu marehemu, tafadhali wasiliana na Abdallah Hussein +27 71 216 8505.

4 comments:

Anonymous said...

Interesting, poleni

Anonymous said...

Why was he buried without the consent of the family

Anonymous said...

mdau wa mwanzo unajifanya mjanja wewe eti interesting mijitu mingine bwana toka wajua kizungu kidogo cha kuombea maji basi wanajifanya wajanja kumbe pumbe tupu kama huna comment ya hekma na busara basi usitume kaa kimya tena ndo utaonekana zinga la msomi ukiwa kimya and a good listener and observer sieti kila kitu kutuma vicomment vya mchwara mchwara

Anonymous said...

wewe anoy wa dec 22 2.27 am, kwanza kwa sharia ya kiislam lazima azikwe si chini ya 24 hrs unless kuwe na mambo ya kihospitali crime labda ilitokana na kifo chake or any strong reason sasa wewe ulitaka waqkae na maiti? na pesa ya kuhifadhia mwili hakuna?unajua mweyewe vijana wengi wanakwendsa south kwa ninikwanza hao waliomzika mungu awajalie,pili namba marehemu alizonazo zote hazifanyi kazi,sasa unataka wafanyeje?tatu possibility ya kuwa hilo jina lake pia ni utata nasema hivyo kwa kua wengi wao hubadilisha majina ili wapate visa au passport.na labda aliacha mawasiliano na familia yake kitambo.Ushauri kwetu sote tusi abandon contact na familia zetu mambo haya hutokea sana huku,communication is a key.Allah amlaze pema peponi.