Mhe. Balozi Tuvako Manongi akizungumza wakati wa mkutano wa pembezoni uliokuwa umeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Elimu, Sayansi na Utamaduni ( UNESCO) na Baraza la Kimataifa la Sayani ICSU), Balozi Manongi alikuwa kati ya wanajopo wanne walioongoza majadiliano hayo.Wengine kutoka kushoto ni Bi. Vibeke Jense ambaye ni Mkurugenzi wa UNESCO Ofisi ya New York, katikati ni mwedesha majadiliano na kulia kwa Balozi Manongi ni Bw. Gisbert Glaser Mshauri Mwandamizi kutoka Baraza la Kimataifa la Sayansi ( ICSU).
washiriki wengine wakifuatili kwa makini majadilianyo hayo kuhusu nafasi ya sayansi na teknolojia katika utekelezaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu, majadiliano hayo yaliandaliwa kwa ushirikiano wa UNESCO na ICSU
sehemu ya wahishiri wa mkutano
Bw. Hassan Mshinda, ambaye ni Kamishna kutoka Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia akichangia katika majadiliano hayo.
Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akibadilishana mawazo na Bw. Gisbert Gladser ambaye katika majadiliano hayo, alitaka kufahamu Tanzania inatumiaje uzoefu wake na mafanikio yaliyoainishwa katika majadiliano hayo kuzisaidia nchi nyingine za Afrika akilenga katika uhusiano na ushirikiano baina ya nchi za Kusini ( South- South Cooperation )
Na
Mwandishi Maalum
Balozi
Tuvako Manongi, Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, amesema, kwa kuwa
sayansi na teknolojia ni suala mtambuka basi tafiti na uvumbuzi unaofanywa na
wanasayansi na wataalamu mbalimbali hauna budi
kujielekeza katika kujibu hoja na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili watu hususani katika kuondokana na umaskini na kujiletea maendeleo endelevu.
Ametoka
kauli hiyo siku ya jumatatu wiki hii,
wakati aliposhiriki katika majadiliano
ya pembezoni ( side event) yaliyokuwa yakijadili kuhusu
‘Sayansi kama tegemeo la baadaye la malengo ya maendeleo endelevu: changamoto na fursa zake zake’.
Balozi
Maongi alikuwa kati ya wanajapo wanne katika majadiliano hayo yaliyoandaliwa kwa pamoja
baina ya Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni ( UNESCO) na Baraza la
Sayansi la Kimataifa ICSU). Wanajopo
wengine walikuwa Mkurugenzi wa UNESCO katika Umoja wa Mataifa, Bi Vibek Jensen, Bw. Gisbert Glaser ambaye
ni Mshauri Mwandamizi kutoka ICSU, na Bi. Paula Caballero, Mkurugenzi wa masuala ya Uchumi, Jamii na Mazingira katika Wizara ya Mambo ya Nje nchini Colombia.
“ Ninapozungumza na wazee wangu kule kijijini
kwangu nilikozaliwa kuhusu athari za
uharibifu wa mazingira kwa kukata ovyo miti, swali wanaloniuliza je unatupa mbadala gani .
Hii ni sehemu ya changamoto ambazo sayansi kupitia kwa wataalamu wetu
wanatakiwa kutoa majibu au kutoa njia mbadala za kuwafanya watu wanaotegemea
miti kwa shughuli zao wasiendele kufanya hivyo” akasema Balozi Maongi
Na kuongeza kwamba Tanzania kama iliyo kwa nchi
nyingine zinazoendelea inaamini kwamba
sayansi na teknolojia inayonafasi
na mchango mkubwa sana
katika kusimamia utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu kutokana
na ukweli kwamba suala hilo linagusa kila nyanja ya maendeleo ya
binadamu.
Hata hivyo akabainisha kwamba licha ya mataifa mengi yakiwamo yaliyoendelea
kukiri umuhimu wa sayansi na teknolojia katika maendeleo, suala hilo halikupewa umuhimu wakati wa
utekelezaji wa Malengo ya Maendele ya Millenia ( MDGs) yanayofika ukingoni
mwaka 2015.
Na kwa
sababu hiyo akasema kwamba Tanzania
ambayo ni miongoni mwa nchi 30 ambazo zimeteuliwa kushiriki katika
majadiliano ya kiserikali ya kuandaa malengo mapya ya maendeleo
endelevu baada ya 2015 (SDGs)
inatajitahidi kuchagiza suala la sayansi
na teknolojia liingizwe katika malengo hayo mapya hasa kipengere cha utekelezaji.
Mkutano huo wa pembezoni umefanyika wakati ambapo
wajumbe kutoka mataifa mbalimbali duniani wapo hapa Makao Makuu ya Umoja wa
Mataifa ( New York) kuhudhuria awamu ya
sita ya majadiliano ya kiserikali , (Intergovenmental negotiations ) kuhuhusu Maandalizi ya Malengo
Mapya ya Mendeleo Endelevu ( SDGs) baada ya 2015
Katika
majadiliano hayo Balozi Manongi
alielezea uzoefu wa Tanzania katika siyo tu utungaji wa será zinazosimamia masuala ya sayansi ya
teknolojia bali hata namna serikali kwa kushirikiana na wadau wa ndani na
nje iliyoweza kupanua wigo wa matumizi
ya sayansi na teknolojia, uongezaji wa ufadhili katika masomo ya juu katika
eneo hilo pamoja na uwezeshaji wa wanawake.
Akataja
pia changamoto mbalimbali ambazo Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine za Afrika inakabiliana nazo, baadhi ya changamoto hizo ni pengo la
teknolojia katika ya mataifa
yaliyoendelea na yanayoendelea,
tatizo la ubadilishanaji wa
maarifa na wimbi la wataalam wa Afrika
kukimbili nje kutafuta maisha bora.
Na kwa sababu
hiyo akasema, pamoja na jitihada mbalimbali ambazo Tanzania imezifanya
na inaendelea kuzifanya katika eneo hilo la sayansi ya teknolojia bado itaendelea kuhitaji misaada na ushirikiano wa karibu hasa katika eneo la uwezeshaji na
ubadilishanaji wa maarifa.
Katika awamu hii ya sita ya majadiliano washiriki wanajikita pamoja na masuala mengine kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu za utekelezaji katika eneo la sayansi, teknolojia, ubadilishaji wa maarifa na uwezeshaji na uhusiano wake na malengo mapya ya maendeleo endelevu
Ujumbe wa Tanzania katika
majadiliano unaongozwa na Balozi Tuvako Manongi ukiwahusisha Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestin
Mush na Bw. Hassan Mshinda ambaye ni Kamishna
kutoka
Kamisheni ya Sayansi na Teknlojia ( COSTECH).
No comments:
Post a Comment