ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 13, 2014

MAPENZI BILA NDOTO NI WIZI MTUPU - 2

TUKIENDELEA na mada yetu, hii ikae kwenye mstari wake ni kwamba lazima mwenzi wako awe wa ndoto zako, kadhalika na yeye vema awe wa ndoto zako. Ni kosa kubwa mtu kuanzisha uhusiano na yule ambaye hana ndoto naye.

Matokeo yake yanakuwa ni migongano na kutotimia kwa malengo ya wahusika. Kuwa na mpenzi ambaye huna ndoto naye ni sawa kumpigia mbuzi gitaa, ukiamini atasikia muziki na kuucheza.

Pengine wewe ndani yako unaona ndoto juu yake lakini yeye hana. Hapa namaanisha kuwa usiishie tu kujitambua wewe binafsi kuwa una ndoto na yeye, badala yake akili yako uishughulishe kutafuta ukweli ndani yake unaokuhusu. Ukishagundua kwamba hana ndoto na wewe, chukua hatua haraka.

Wengi walichukuana, wakajitahidi kuyajenga maisha pamoja lakini hawakufika popote. Inawezekana hata mke na mume kuingia kwenye ndoa lakini bado ikawa hakuna matunda chanya. Ukiona ndoa ina misuguano miaka nenda rudi, chunguza halafu utagundua kuwa wahusika hawakuwa na ndoto.

Mke na mume wanakuwa na balaa la usaliti! Mke anachepukia kule, mume anajirusha kivile. Kama wahusika wangekuwa na ndoto za kuishi pamoja, halafu ndoto hiyo ndiyo ingetumika kuwafanya wachumbiane kabla ya kuoana, heshima ingekuwepo.

Usaliti, ukosefu wa uvumilivu, kutoheshimiana na mambo mengine kama hayo, ni matokeo ya kukosekana kwa ndoto baina ya wawili waliotamkiana kuwa wanapendana. Mtu wa ndoto zako huwezi kumsaliti. Vivyo hivyo, ungekuwa wa ndoto zake asingekusaliti.

Kama wewe ni wa ndoto zake ni lazima akuvumilie na akuheshimu hata kama jambo ulilomkosea ni kubwa kiasi gani. Hii ni kwa sababu, pamoja na maudhi ambayo unampa lakini upo ndani ya mawazo yake, kwenye usingizi wake. Hawezi kukuacha, ndoto itamlazimisha aendelee kuwa nawe.

Dunia ya leo, watu wanakurupuka kuchumbiana. Nyakati nyingine hata uhusiano wao hautambuliki kwa wazazi lakini wanaitana wachumba. Unafika muda wanakuwa pamoja, inakuwa haiwezekani kuwashauri vinginevyo, maana wao wanasema wanapendana sana. Tatizo ambalo hawalibaini ni ndoto!

NGUVU YA NDOTO
Haitakuwa mara yako ya kwanza kusikia kuhusu mwanaume kujitoa kikamilifu kwa mpenzi wake. Alimsaidia kwa kila hali, akampeleka shule, akalipa mahitaji yote muhimu. Imani yake ni kwamba baada ya masomo, watakuwa pamoja na kufunga ndoa na kuishi kwa furaha yakinifu.

Mwanamke baada ya kuhitimu masomo anaamua kujichenga kwa mwanaume mwingine, yule aliyemsomesha na kumuwezesha huduma zote

GPL

No comments: