Na mshindi ni …. Cristiano Ronaldo. Usiku wa leo jijini Zurich, FIFA itamtangaza nyota huyo raia wa Ureno kuwa mwanasoka bora wa dunia kwa mwaka 2013 ambayo itakuwa tuzo yake ya pili.
Cristiano Ronaldo amepata kura nyingi zaidi ya wapinzani wake Franck Ribéry na Leo Messi, kwa kushinda tuzo hiyo Ronaldo atakuwa ameusitisha ufalme wa Messi aliyekuwa ameishinda tuzo hiyo kwa miaka 4 mfululizo.
Chachu ya ushindi huo wa Ronaldo ni mabao 69 aliyofunga mwaka 2013, ikiwa ni pamoja na kuumaliza mwaka vizuri.
Ronaldo mwenyewe anajua kuwa ni mshindi tangu juma lililopita baada ya kudhibitisha kushiriki kwenye sherehe za tuzo hizo, pamoja na kushiriki Ronaldo amewapa mialika ndugu na rafiki zake wa karibu,mpenzi wake mwanamitindo Irina Shayak wakala wake Jorge Mendes.
Pia wapo viongozi mbali mbali wa Real Madrid akiwepo raisi Florentino Pérez, Emilio Butragueño, Zinedine Zidane na Sergio Ramos, ambaye atatangazwa kuwa beki bora wa kati sambamba na Mbrazil Thiago Silva.
No comments:
Post a Comment