DIWANI HAILE NYUMA MWENYE SUTI NYUMA AKITOKA MAHAKAMANI |
ASKARI MAHAKAMANI
DIWANI
wa Kata ya Kitaji Manispaa ya Musoma Haile Tarai (Chadema) pamoja na
watu wengine watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa
wakidaiwa kumfanyia fujo Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya CCM(NEC)
Vedastus Mathayo katika msiba wa Shekh wa mkoa wa Mara Athumani Magee.
Mbele ya
Hakimu Mkazi Mwandamizi Faisal Kahamba,imedaiwa na mwendesha mashitaka
wa polisi Jonas Kaijage mnamo January 30 mwaka huu watu hao
walimsababishia usumbufu na fujo ambazo zingeweza kuhatarisha amani
miongoni mwa jamii wakati Mathayo akiwa ndani ya gari aliyokuwa
akiendesha mwenyewe kuelekea kuhani msiba.
Washitakiwa
hao walidaiwa kutenda kosa hilo kinyume na kanuni ya adhabu kifungu cha
171(a) sura ya 16 ya mwaka 2002 na kufunguliwa kesi namba 31 ya mwaka
2014
No comments:
Post a Comment