ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, February 2, 2014

HAFLA YA KUMUAGA RASMI KAMISHNA JENERALI ALIYESTAAFU WA MAGEREZA NCHINI NAMIBIA

 Kamishna Jenerali wa Magereza Mstaafu  Evaristus Shikongo (amesimama katika Jukwaa) akitoa hotuba fupi mara baada ya kukabidhi rasmi Madaraka ya Uongozi wa Jeshi la Magereza Nchini Namibia  kwa Kamishna Jenerali Mpya wa Jeshi la Magereza Raphael Hamunyela.
 Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali Mpya wa Jeshi la Magereza Nchini Namibia, Raphael Hamunyela(wa pili kushoto), Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria, Evaristus Shikongo(wa pili kulia), wa kwanza kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Uganda.
 Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja (kulia) akitoa hotuba fupi wakati wa hafla ya kumuaga rasmi  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Evaristus Shikongo ambaye amestafu Utumishi wake wa Umma kwa mujibu wa Sheria.
 Kamishna Jenerali wa Magereza Mstaafu wa Namibia, Evaristus Shikongo akiwa ameshika Saa ya Ukutani aliyokabidhiwa na Naibu Kamishna wa Magereza Mstaafu, John Nyoka(kulia) ambaye alifanyanae kazi Nchini Namibia kama Mtaalamu wa masuala ya Uendeshaji wa Programu za Urekebishaji Magerezani kutoka Jeshi la Magereza Tanzania kufuatia Makubaliano Maalum na Serikali ya Tanzania(kushoto kwa Jenerali) ni Mke wa Kamishna Jenerali wa Magereza Mstaafu wa Namibia.

Wasanii wa Bendi ya Jeshi la Polisi Nchini Namibia wakitumbuiza mbele ya Wageni Waalikwa(hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumuaga rasmi aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia kufuatia kustaafu kwakwe Utumishi wa Umma. Sherehe hizo zilizofana sana zimefanyika Februari 01, 2014 katika Ukumbi wa Chuo cha Maafisa Magereza cha Omaruru kilichopo nje kidogo ya Mji Mkuu wa Windhoek, Namibia(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments: